Tundu Lissu 'Kwa Hili La Mchanga wa Madini Tutanyolewa Bila Maji'


Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu ameibuka na kuishauri serikali jambo la kufanya kutokana na matokeo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliofanywa na kamati ilyoundwa na Rais John Magufuli.

Tundu Lissu anasema Tanzania ni mwanachama wa 'The MIGA Convention' hivyo ukiwa mwanachama ukachukua mali za wawekezaji wao utapelekwa kwenye mahakama za kimataifa na kwenda kushughulikiwa huko, hivyo Tundu Lissu ametoa ushauri wa namna nzuri ya kushughulika na watu

"Sisi Tanzania ni wanachama wa kitu kinaitwa 'The MIGA Convention' Multilateral Investment Guarantee Agency ya benki ya dunia, ukiwa mwanachama wawekezaji wakileta mali zao kwako, ukichukua mali zao kama walivyochukuliwa mali zao namna hii utapelekwa kwenye mahakama zao za kimataifa unaenda kushughulikiwa huko, tumesaini mkataba wa ulinzi wa wawekezaji na mataifa wanayotoka wawekezaji hao Marekani, Canada, Uingereza wote ni mabosi wakubwa makampuni ambayo Rais ameyakamatia mali zao yanatoka kwenye hizi nchi tuna 'bilateral investment treaties ambazo zinalinda mikataba hii" alisema Tundu Lissu 


Tundu Lissu anasema hili suala tusipokuwa makini nalo linaweza kuleta matatizo makubwa huku akimtaja muhusika wa mikataba iliyolifikisha taifa katika hasara iliyobainika katika uchunguzi huo.
"Rais anajiingiza kwenye mgogoro mkubwa, akimkamata Dalali Kafumu peke yake, tutamwambia kwanini siyo Gray Mwakalukwa mikataba yote hii imeingia wakati wa Mr. Gray Mwakalukwa, kwanini siyo Daniel Yona, kwanini siyo Jakaya Kikwete sababu alikuwa Waziri na mimi nina mkataba wa Bulyankulu na kwanini siyo mawaziri wote, kwa sababu mikataba iliingiwa wakiwa mawaziri" alisema Tundu Lissu 

Lakini mbali na kusema yote hayo Tundu Lissu alitoa ushauri wake katika suala hilo...

"Kama unataka kufanya haya unayoyafanya elewa hali halisi ilivyo, tatizo liko wapi kama tatizo ni kwamba tunapata mapato kidogo na kweli wanatupiga kweli kweli ila kama utaka kufanya mambo kweli kweli kajiondoe kwanza MIGA ili hao wawekezaji wasikushtaki kwenye hizo mahakama za huko, maana wakikushtaki kule unanyolewa bila maji, hakuna ndege ya Tanzania itakanyaga hizo nchi wataikamata, hakuna hela tutaweka kwenye nanii za kimataifa watazikamata, kwa sababu tunavunja mikataba ya kimataifa inayolindwa na sheria za kiwekezaji za kimataifa, kwa hiyo anzia huko juu ukimaliza mikataba ya kimataifa, njoo kwenye mikataba kati ya nchi na nchi ondoa hiyo mikataba ukishaondoa hiyo hushtakiki nje, baada ya hapo njoo ndani sababu bado unaweza kushtakiwa ndani" alisisitiza Tundu Lissu 

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Bernard Manyano25 May 2017 at 17:01

    Mh Lissu anakosa mantiki.... Kwanini nasema hivi

    Kwa mtiririko wake kama hoja/nia ya Mh Rais ni kupokonya wawekezaji mali zao yaaani mpangilio wa Mh Lissu ungekuwa ni sahihi sana✅

    Ila sasa mtiririko huo anapotosha na kukosa mashiko kwani dhamira ya Mh Rais juu ya zoezi hili la mchanga ni *kujua thamani halisi ya mchanga ule* ili kama nchi tuweze kupata fair deal hata kwa hiyo hiyo 4percent...tukumbuke tunapoteza almost 630bil kwa mwaka just from mahesabu ya tume's (1.44tril) na Acacia (112.1bil) kwa mwezi kwa 4percent yetu ya sasa.

    Sijasikia sehemu Mh Rais anasema Acacia wapokonywe mgodi au kufungia kazi zao hapa nchi au ule mchanga utaifishwe. Anacho sisitiza Mh Rais ni kuwa tunabiwa....

    Jamani msituchanganye...�� Just this once msaidie Rais... Hili jambo linatuhitaji sisi sote kushikamana kama nchi bila kujali vyama.

    Sioni kabisa The MIGA convention inakujaje hapo wakati hupokonyi chochote... Hembu nisaidieni katika ku connect the dots

    I'm confused

    @Manyano

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad