Lissu alisema ni muda mrefu walimwandikia barua Rais Magufuli kutaka kukutana naye kwa ajili ya uongozi mpya kujitambulisha rasmi kwake na kufanya naye mazungumzo.
“Tunasubiri ajibu barua yetu kwa kuwa tulishaomba kukutana na Rais Magufuli tuzungumzie utawala wa sheria,” alisema Lissu.
“Tunafahamu yuko busy (ana shughuli nyingi), lakini atenge muda hata nusu saa au saa nzima ya kuongea na kiongozi wa chama cha mawakili wa Tanganyika,”
Alisema lengo kubwa ni kujitambulisha na kuzungumzia utawala wa sheria na mwelekeo wa Taifa. Pia, ana imani kwamba Rais atawakaribisha.
Kiongozi huyo wa wanasheria alisema watakachokifanya ni kumweleza maoni ya TLS na pale watakapoona amekosea, hawatasita kumweleza na anapoona kuna matatizo awe huru kuwaeleza. Alisema Rais akikubali itakuwa ni vizuri kwa sababu ni maongezi ya kawaida kwa lengo la kuimarisha TLS na kujitambulisha kwake.
Lissu, ambaye pia ni mbunge wa Singida Mashariki alichaguliwa kuwa rais wa chama hicho mwezi uliopita na Rais ni mmoja kati ya viongozi kadhaa ambao TLS imewaandikia kuomba kukutana nao.
Aliwataja wengine kuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Kaimu Jaji Mkuu, Mkuu wa Jeshi la Polisi na marais wawili wastaafu; Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete. Amesema tayari Kaimu Jaji Mkuu ameshakubali ombi lao.
Pale uliposema "utainyoosha serikali ya Magufuli" tayari umeshatangaza 'uadui', wewe fanya yako tu, JPM hataki shobo zako.......USIJIPENDEKEZE mfyuuuuuu....HAPA KAZI TU!!
ReplyDelete