UKWELI Mchungu ..Msiba na Namna ya Kumsindikiza Marehemu, Utamaduni Uliozoeleka...!!!


'waache wafu wawazike wafu wenzao' maneno haya ya kwenye maandiko yanamaanisha hatutakiwi kuhangaika sana na wafu au marehemu kwa sababu wameshamaliza muda wao na hakuna kitu kinachoweza kuongeza thamani yake au kupunguza aliyokuwa nayo wala kufanya chochote juu yake kitakacho punguza makosa yake au kuongeza. Akishafariki ni kuzika mara moja.

Zipo tamaduni mbalimbali za kumsindikiza marehemu katika nyumba yake ya milele. 

Waislam huzika siku hiyo hiyo wenda itokee sababu iliyo nje ya uwezo na kusababisha kuzika kesho yake. 

Wakristo hukaa na msiba hadi siku 5 inategemeana tu na sababu nyingi kama uwepo wa ndugu n.k lakini kiufupi hukaa na msiba siku nyingi sana. 

Nimeainisha utaratibu huo katika makundi hayo lakini sidhani kama kuna haja ya kukaa na marehemu kwa muda mrefu sana najua inauma sana lakini ameshakufa ni vizuri kumpumzisha mapema. 

Napenda sana utaratibu wa kiislamu wa namna ya kudeal na msiba. Hawakai nao na huzika haraka lakini kwa namna ya kikristo hukaa na msiba muda mrefu ambapo si vizuri kwanza unaongeza gharama na kuingia gharama kubwa kulisha au kwa namna yoyote kuugharamia hadi muda wa maziko ufike, pili unaongoza uchungu na huzuni kwa waombolezaji na hii yatokana na mawazo yaliyopo juu ya uwepo wa mwili kabla ya kuzika na mwisho, muda wa kushughulika na msiba waweza kupoteza opportunity zingine za kuwaongezea kipato au kupoteza mapato kutokana na kufunga biashara muda mwingine. 

Katika makundi hayo juu, wapo wengine ambao huonesha utamaduni mzuri ambao hawaweki matanga kwa siku nyingi pia hata namna ya kuzika hawakusanyiki wengi wanakuwa wachachekwa ujumla suala la kumpumzisha marehemu huwa rahisi na la muda mfupi na wamalizapo huendelea na shughuli kama kawaida. Mifano ipo mingi lakini twaweza kuangalia desturi kwa white men (western culture). Tunaweza kuwaita wabinafsi na wachoyo kwa kulinganisha namna zetu za kushughulika na misiba lakini naamini yaweza kuwa njia nzuri na rahisi isiyokuwa na gharama kubwa wala ugumu kuikamilisha. 

Nadhani kuna haja ya kubadilisha utamaduni huu ili kuenzi maneno ya wafu kuwazika wafu wenzie. Kufanya sehemu ya msiba sio ya watu kushinda bali kutoa pole na kwenda kuzika then kila mtu kugawanyika. Kwa kufanya hivyo twaweza okoa mambo mengi. 

Waweza kuwa na maoni tofauti ila yangu ni haya. Ni jambo la huzuni na linauma lakini sio lazima likafanyika kutokana na mazoea. Sorry kwa nitakao wakwaza.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad