Hatua aliyoichukua Rais juu ya swala hili la Mchanga wa dhahabu ni kitendo kilichoonesha umakini na nia ya dhati ya serikali kusimamia rasilimali zetu hivyo kuongeza imani waliyokuwa nayo wananchi juu ya awamu hii ya uongozi.
Wakati hilo likitokea kitendo hicho cha rais ni moja ya misumari muhimu itakayosiliba kabisa matumaini ya wapinzani.
Kauli za baadhi ya wapinzani katika kukosoa kitendo hiki cha kizalendo ni matokeo na hasira za kupunguziwa hoja za kuinenea mabaya serikali.
Ni jambo lililowazi kuwa mambo hayakuwa sawa huko migodini wengi walilalamika hilo limedhihirishwa na matokeo ya kamati ya wataalam aliyoiunda Rais.
Ila baada ya juhudi hizo za wazi kuonesha mwanga wa utatuzi wa malalamiko yetu ya muda mrefu; wale wale waliokuwa kati ya walalamishi wameanza kugeuka kauli zao na kuanza kutuambia kwamba kilichofanyika ni makosa eti tutapata hasara kama Taifa.
Kauli hizo na nyingine nyingi toka upinzani zinatufanya baadhi yetu tuanze kujiuliza lengo halisi la upinzani hapa nchini ni nini?
Je malengo ya upinzani ni kuibua mabaya tu ili kupata umaarufu?
Je; serikali inatakiwa kukosea tu kila mara ili ikosolewe na upinzani?
Je; serikali haina haki ya kufanya mambo sahihi kwa watu wake?
Je; ni upinzani pekee ndio wenye haki ya kufanya mambo sahihi kwa wananchi.
Je; ni lazima upinzani ukosoe hata yale mazuri ya serikali?
Mwisho wa yote fikra zinamuongoza mtu kuona kama jambo hili jema limepunguza kete za upinzani na upinzani hawajalifurahia kwakua wanakosa agenda za kwenda nazo kwa wananchi.
Na fikra hizo hizo zinakutuma kuona kwamba upinzani wamekosa uzalendo na zaidi sana wanawaza umaarufu wao.