Godbless Lema akizungumza bungeni alisema viwanda ndiyo imekuwa ajenda kubwa ya serikali ya awamu ya tano lakini kiwango cha fedha zilizopelekwa ni kidogo sana hivyo anaona hakiwezi kufanya mabadiliko na kuleta viwanda nchini.
"Serikali imekuwa ikipigia sana kelele kuhusu suala la viwanda lakini katika bajeti inayoishia kati ya bilioni 42.1 serikali ilipeleka bilioni 7.6 asilimia 18 tu ndiyo maana Mh Mwijage anavyosema cherehani nne ni viwanda halafu watu wakimshangaa mimi nawashangaa hao wanaomshangaa, ni ukweli viwanda vya serikali ya awamu ya tano ni cherehani nne. Mh. Mwenyekiti hii ndiyo ajenga kubwa ya serikali ya wamu ya tano viwanda kati ya bilioni 42 mnapeleka bilioni 7 hamtaweza kuibadili hii nchi kwenda kuwa taifa la viwanda" alisema Lema
Mbali na hilo Mbunge huyo aligusia pia suala la maji na kusema maji ni hitaji muhimu kwa kila binadamu hivyo serikali ingeweza kuona hiyo fursa na kutengeneza miundombinu mizuri ili ijipatie pesa kupitia maji.
"Maji ni biashara Mh. Mwenyekiti najiuliza kwanini nchii hii haijawahi kuona maji ni biashara, tena maji ni biashara ambayo haihitaji matangazo sababu kila mtu anahitaji maji mahitaji namba moja ya binadamu anayeishi ni maji, mmeshindwa kutengeneza mipira, mmeshindwa kutengeneza miundombinu mizuri na kuweka mita ili serikali iweze kukusanya fedha kutoka kwenye maji, kama hatujaweza kuona kuwa maji ni biashara cherehani nne lazima zitakuwa ni viwanda" alisisitiza Lema