Akiongea na Bongo5 Jumamosi hii msemaji wa label hiyo, King Maarifa, amedai wao hawawezi kumchukua mtu ambaye anatumia dawa za kulevya na kufanya naye kazi.
“Tumezisikia hizo tuhuma juu ya msanii wetu na sisi tumezipokea kwa namna mbili, moja sisi kama sisi tunajua Young Dee aliacha kutumia dawa za kulevya na baada ya sisi kuhitaji kufanya naye kazi tulimchunguza vizuri kwa kipindi cha miezi 5 na tumejiridhisha hatumii tena. Sisi tunachokijua Young Dee na uongozi wake uliopita walishindwa kuhafikiana baadhi ya mambo, hayo mambo ya dawa za kulevya ndio kwanza tunayasikia kwake,”
Aliongeza,
“Sisi tumeingia kwenye hii biashara kwa miguu miwili. Kwa hiyo tunavyomsikia mtu akiizungumzia vibaya brand yetu kamwe hatuwezi kukaa kimya, tunaomba aachane na hayo mambo, hatutaki kufikishana mbali zaidi kwa sababu tayari ameshatoka kwake. Pia sisi mwanzo tulijua kwamba baada ya kusikia tumesaini naye atakuja kutoa mikataba kueleza kwamba ana mkataba na Young Dee, sasa tunaposikia hizo tuhuma tunaanza kupata shaka sana juu ya hizo kauli zake,”
Hapo awali Young Dee akizungumza na Clouds FM, alidai aliondoka katika uongozi huo baada ya meneja wake huyo kutembea na mpenzi wake aitwae Tunda.
Hata hivyo meneja wa label hiyo, Max Rioba alikanusha taarifa hizo nakudai aliachana na rapa huyo baada ya kurudia kutumia dawa za kulevya.
Mwaka uliopita rapa Young Dee mbele ya waandishi wa habari alitangaza kuacha kutumia dawa za kulevya baada ya kutumia kwa kipindi cha miaka 2.