HALI za wanafunzi majeruhi wa shule ya Lucy Vincent ya mkoani Arusha, waliopelekwa hospitali ya Mercy jijini Sioux katika jimbo la IOWA nchini Marekani kwa matibabu inaendelea vizuri na tayari wote watatu wamefanyiwa upasuaji.
Majeruhi Sadya Awadh na Wilson Tarimo wote walifanyiwa upasuaji jana wakati Doren Mshana alifanyiwa juzi. Mtu wa Karibu anayefuatilia afya za watoto hao na Mbunge wa Singida Kaskazini na rafiki wa karibu wa watalii madaktari waliowaokoa majeruhi na kuopoa maiti siku ya ajali Mei 6, mwaka huu.
Ajali hiyo ilitokea katika eneo la kilima cha Rhotia, Karatu na kusababisha vifo wanafunzi 32 wakiwemo walimu wawili wanafunzi na dereva, aliandika hayo katika ukurasa wake wa Facebook jana.
Nyalandu alisema: “Kila mtoto amewekwa kwenye chumba chake peke yake, na mama mzazi na muuguzi mmoja wanakuwa naye wakati wote.” Mbunge huyo alisema Sadya amefanyiwa upasuaji maeneo matatu yaliovunjika ikiwemo mkono wa kulia lakini shingo haikufanyiwa upasuaji na badala yake aliwekewa kifaa cha kunyoosha (Brace) atakayokaa nayo wiki sita kuanzia sasa.
“Wote wanaendelea na mapumziko katika hospitali ya Mercy, Sioux City. Mungu ni mwema sana,” aliandika Nyalandu. Katika hatua nyingine, kutokana na ajali hiyo, Polisi wa mkoani humo limetangaza kiama kwa kuyakamata magari yote mabovu yasiyokidhi viwango vya kusafirisha wanafunzi yanayotumiwa na wamiliki wa shule za watu binafsi Jijini hapa.