Ushauri kwa Tundu Lisu Juu ya Makontena ya ACACIA...!!!


*Ushauri kwa _Tundu Lisu_*

Ukiwa Kama mwanasheria mashuhuri nakuomba ulisaidie Taifa na hawa mapepari na majizi ya rasilimali zetu wanaojiandaa kwenda kulishitaki Taifa letu kwenye Mahakama za kimataifa kisa tu Taifa limechukua hatua kwa namna tunavyoibiwa rasilimali zetu na hao mapepari wanatumia mgongo wa sheria tena walizotunga wao na zinabeba hao hao kuendelea kutunyonya kwa kigezo cha Mahakama za kimataifa. 

Ni kweli kutokana na sheria za kimataifa zilivyokaa ikitokea ACACIA wakaenda mahakamani Taifa litawalipa fidia kubwa sana, pesa ambazo ni kodi za sisi wananchi wa hali za chini. Ifahamike kuwa hawa wawekezaji wanatuibua kwa kutorosha rasilimali zetu wakijua mwisho wa siku kuna sheria za kimataifa zilizotungwa na hao hao zitawatetea tena. Kwa lengo la kizalendo nakuomba Tundu Lisu Ukiwa Kama Rais wa TLS na pia Mtanzania mwenzetu andaa timu yako ya wanasheria mahili (Akina Malya, Mabere Malando, Chenge) na wengine wengi kuhakikisha mnaenda kupambana nao huko kwenye Mahakama zao wanakopanga kwenda kulishitaki Taifa. 

Kwa hili la rasilimali zetu tuweke uvyama pembeni tuungane kumuunga mkono Mh Raisi kwa hatua alizochukua. Ni kweli kabisa bado Kuna changamoto nyingi kwenye uwekezani wa rasilimali zetu haswa katika upande wa mikataba na sheria mbovu zinazosimamia hiyo mikataba iliyosainiwa na viongozi wetu ambao pia ni Watanzania wenzetu (wengine bado wapo madarakani eg. Akina Chenge kipindi hicho akiwa mwanasheria mkuu wa Serikali) . 

Hivyo basi kwa hatua za awali hawa wanaojiita wawekezaji tukiwashinda kwa hili la mchanga hayo mengine ya mikataba kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu siku moja pia tutayafikia tu. 

*UKWELI HUWA UNA ASILI YA KUUMIZA, ILA KWA HILI LA RASILIMALI ZETU TUSIMAME UPANDE WA UKWELI*

Chanzo jf

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tanzania Africa kiujumla.Kwanza Bara la Africa halijaungana kwa hiyo hakuna hata sauti ya kutetea mali asili zao. Na ndio bara linawatajilisha nchi matajiri. waendelee kuwa matajiri na Africa eiendeler kuwa masikini na kingine ujinga wa Viongozi wetu. Sijui ni ulimbukeni wakishaonyeshwa vihela kidogo wao wanasini tu mikaba mradi apate cha mfukoni.Wacha waendelee kuitwa watu wenye 1Q ndogo. Interigent Qurity sawa karibio na ziro.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad