1. Tanzania inapaswa kusitisha au kujitoa kwenye Makubaliano ya Kimataifa kuhusu usuluhishi au uamuzi wa migogoro ya kimataifa. Hii itawazuia watakaoguswa kwenda nje kutushtaki na kutubabaisha.
2. Sheria zote za zinazohusu madini na nishati zipitiwe upya na kurekebishwa ili kulinda maslahi ya nchi. Itakuwa ni nafasi ya kurekebisha mrabaha na maslahi mengineyo
3. Mikataba yote ya madini na nishati ifumuliwe na kusukwa upya kwa lengo kama la kwenye nambari 2. Mikataba itamke wazi usuluhishi au uamuzi juu ya migogoro ufanyike katika Mahakama za Tanzania au kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.
4. Serikali ya Tanzania inapaswa kuwa na hisa katika kila kampuni ya madini au nishati. Hili lielezwe vyema kwenye Sheria na Mikataba.
5. Kuwepo na timu imara za majadiliano za Serikali kuhusu madini na nishati na vyombo vya usalama vihusishwe kumulika nchi hizo.