Simu moja aina ya smartphone imechukua jukumu muhimu katika majaribio ambayo huenda yakasaidia mamilioni ya watu duniani ambao wanakabiliwa na ugonjwa wa kisukari ili kuweza kuthibti kiwango cha sukari.
Watafiti wa China katika jarida la sayansi wanasema walivumbua seli za insulini na kuzidunga ndani ya panya ili kufanya kazi wakati zinapoangazwa na mwanga wa LED.
Mwanga huo ulizalishwa na programu ya simu hiyo aina ya smartphone baada ya kupokea data kutoka kwa kifaa cha kupimia damu ilio na sukari ndani ya panya huyo.
Kwa sasa watu walio na kisukari hupimwa damu ili kubaini ni wakati gani wanahitaji sindano za insulini.