Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema amesikitishwa na hatua ya Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam ya kuzuia kongamano la demokrasia lililopangwa kufanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Anatouglou.
Lowassa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alitoa kauli hiyo leo (Jumamosi) wakati akizungumza na wanahabari ofisi kwake Mikocheni.
Amesema amelaani kitendo hicho na kusema kongamano hilo halikuwa na nia mbaya bali lilikuwa limelenga kujadilia mambo mbalimbali kwa mustakabali wa Taifa.
"Nimesikitishwa na kitendo hiki na nimeshangaa kwa jambo hili halikemewi.Nchi hii ni moja na kila mtu ana haki.
"Walituzuia mikutano ya hadhara tumetii, tumeamua kufanya mikutano ya ndani wanatufuata fuata,"amesema Lowassa ambaye aliwahi Mbunge wa Monduli kwa nyakati tofauti.
Katika mkutano huo Lowassa aliambatana na mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi ya kongamano hilo Dk Makongoro Mahanga ambaye alishangazwa na hatua hiyo ya Serikali ya mkoa wa Dar es Salaam