WAITARA Awekwa Mtu Kati Bungeni..Akubali Yaishe Baada ya kukosea Kuasilisha Hotuba..!!!


Bunge limembana Naibu Waziri Kivuli wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mwita Waitara na kulazimika kufuta baadhi ya maneno yaliyokuwa katika hotuba ya kambi rasmi ya upinzani bungeni kuhusu bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/18.

Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu amembana Waitara baada ya mwongozo ulioombwa na Waziri wa Nchi,  Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama mara baada ya bajeti ya wizara hiyo kupitishwa na Bunge.

Mambo yalianza kwenda kombo kwa Waitara wakati Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi alipokuwa akihitimisha hoja yake kumtaka naibu waziri huyo afute kauli zake zinazodaiwa kuwa za uongo au azithibitishe kabla ya kuombewa mwongozo na Mhagama.

 “Kauli kama hizi zinasababisha kupandikiza mbegu za utomvu wa nidhamu jeshini. Narudia nimesikitishwa sana na maneno yenye lengo la uwagombanisha wanajeshi na Serikali yao na uongozi wao wa juu. Hii halipwaswi kuvumiliwa na ni vyema Bunge lako liangalie utaratibu wa kumtaka msemaji wa kambi hii ya upinzani athibitishe maneno yake,”amesema.

Hata hivyo, baada ya kubanwa sana na Zungu, Waitara alitamka kuwa ameyafuta maeneo hayo na maneno ya Dk Mwinyi ndio yachukuliwe kuwa ya ukweli.

“Kwa heshima na taadhima naomba kufuta maneno hayo, tuko pamoja,”amesema Waitara.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad