WAKOLONI Wamechangia Umaskini Afrika - Kikwete Afunguka

Aliyekuwa rais wa Tanzania awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete,amesema koloni za mataifa ya Afrika yamechangia kujikokota maendeleo Afrika kwasababu ya kutotoa usadizi wa aiana yeyote ikiwemo kuwanyima elimu waafrika wengi katika maeneo waliyoyatawala.

Dkt Kikwete amesema hayo katika Mkutano wa kiuchumi Duniani -World Economic Forum kwa Afrika mjini Durban Afrika Kusini, lengo hasa likiwa kutafuta namna za kukuza uchumi wa Afrika.
Rais huyo wa zamani amesema tayari serikali za mataifa mbalimbali Afrika zimechukua hatua katika kuboresha elimu katika mataifa yao kuanzia shule za chekechea,msingi na hata vyuo vikuu ili kupunguza idadi ya watu wasio na uwezo wa kusoma na kuandika katika kujiletea maendeleo

Ameongeza kuwa nchi zinapokabiliwa na mahitaji makubwa elimu matatizo yanajitokeza na hiyo ni kwasababu nchi nyingi zilianzia chini sana na uwekezaji wote huu uliopo sasa katika bara la Afrika umefanyika baada ya nchi hizi kupata uhuru.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Maraisi Wa Afrika mnauhuru, Uwezo, wa kubadili hili. Kuelimisha Waafrika, Watanzania. Kuwaheshimu Wasomi wa Africa kwanza, kuwapa fursa na kuwasaidia kiuwekezaji.
    Kutawala kwa kufuata sheria na katiba zinazotawala na kulinda nchi.
    Kuto kuwapa fursa hao watu, Mnajua hasa hawapo na nia njema ya kuendeleza Africa, Tanzania.
    Nia zao mnazijua hasa ni kuucontroll uchumi wetu na kuona utajiri walionao hauhuki. Ni Africa inawafeed wawe matajiri zaidi na cuucontroll uchumi duniani.
    Bado hamjaondoa vikwazo vya biashara vyote vilivyowekwa nao. Mfano kupeleka kahawa kwenye soko la Arusha auction. Kwa nini Mtanzania mwenye uwezo asiuze kahawa nje direct. Unawaachia watawale soko hilo kidunia, mbona hawapeleki mazao yao auction kama tunavyofanyishwa sisi.
    Mnawakubali kuja kupitia non profit kuibia wananchi kuwatengenezea vitu kwa bei ya chini sana vijijini kwetu . Wengine hata vibali hawana.
    Kuwaingiza watumie ardhi yetu na kujilimia mazao yanayopelekwa kwao. Kwa nini msiwasaidie Wakulima walime viazi na kuuza Japan. Mnatufanyisha kazi, mnatoa maeneo bora ya kilimo mali ya Watanzania kwao, je mtaliingiaje soko lao na tukafaidika wananchi kwa uamuzi wenu mbovu.
    Ubinafsi wa viongozi wetu, na kunyimwa uhuru kwa kuwashirikisha Wananchi waamue knamna gani watumie raslimali zao badala ya kuamua watu ikulu.
    Elimu, Sheria bora, Uhuru, uwezo wa kufikiri, Kujiamini na kujituma. Kunegotiate mikataba kama ya gesi ambayo mingi na ya maduni ni wizi mtupu, na mnashindwa kuinyang"anya ni ktutuletea umaskini. inferiority complex zetu kwa kukosa kujiamini na kutoweza zungumza vizuri ni vikwazo vikuu.
    Haya matatizo yanasababishwa na sisi wenyewe kwa namna hizi.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad