Wastara Awaburuza Wasambaza Filamu Bongo Kortini


STEPS Entertainments, ambayo ni kampuni ya kusambaza filamu Tanzania, imepelekwa mahakamani na Wastara Juma, anayeidai kiasi kikubwa cha fedha baada ya kukataa kumlipa, Risasi Jumamosi limeambiwa.

Kwa mujibu wa chanzo, muigizaji huyo alipeleka kazi yake kwa kampuni hiyo ili asambaziwe kama wanavyofanya waigizaji wengi nchini, lakini licha ya kusubiri kwa muda mrefu, kampuni hiyo imeshindwa kumlipa na hivyo kumfanya kuamua kuipeleka kortini.

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Wastara alikiri kuchukua hatua hiyo akidai amewapeleka katika Mahakama ya Mwanzo Ilala akitaka apewe fedha zake alizokataa kutaja kiasi chake, lakini akisema licha ya kupewa barua mbili za kuitwa mahakamani, hawajawahi kufika.

“Hapa ninavyoongea napewa barua ya tatu kwa ajili ya kuwapelekea, wasipofika tena mahakamani mali zao zitakamatwa na kupigwa mnada ili wanilipe,” alisema.

Juhudi za kuwatafuta wahusika wa Steps ziligonga mwamba baada ya msemaji wao, aliyejulikana kwa jina moja la Moses kutokuwepo ofisini, ingawa ofisa mmoja wa kampuni hiyo aliyeomba hifadhi ya jina lake, alikiri kampuni hiyo kudaiwa na kupokelewa kwa barua za Wastara.

“Mimi si msemaji, mwenyewe yupo lakini habari za Wastara kuleta barua nimezisikia, -ila jitahidi umuone hata mwanasheria wetu Cloud atakupa ukweli ulivyo,” alisema ofisa huyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad