WAZIRI Muhongo: Mikataba Yote ya Umeme Nchini ni Mibaya..!!!


Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo amewataka watanzania kukubaliana na ukweli kuwa mikataba yote ya umeme iliyopo hapa nchini ni mibaya. Waziri Muhongo ameyasema hayo alipokuwa akijibu changamoto zilizoelekezwa katika Wizara yake katika Mkutano wa Baraza la Taifa la Biashahara, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Hatahivyo,Waziri Muhongo hakufafanua kuhusu wahusika wa mikataba hiyo;mikataba husika na namna ya kuifanya iwe mizuri. Mtakubaliana nami kuwa mikataba ya umeme kati ya TANESCO na Makampuni ya kuzalisha umeme imekuwa ikizalisha kashfa za kifisadi pamoja na kesi mbalimbali za jinai na madai kwa miaka mingi sasa.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Muhongo ni wewe chanzo cha mikataba mibovu na serikali ya CCM kwa miaka mingi. Upinzani umlifanya juu chini kuibua swala hili hasa Chadema na Zitto kabwe pia Kafulila. Mmepeana pesa, mmlianzisha makampuni hewa, .mlitumia uongozi wa Kikwete kuibia na kudanganya Watanzania. Ni aibu kiongozi msomi kama wewe kutumika na serikali, chama, na kuhadaa watanzania wote. Usomi kama huu, ni limbikizo la maendeleo barani Afrika. Uchumi wote wa nchi, mikataba yote ikuu ya madini smbayo mmewapa wazungu kwa miaka yote pia ni wizi. Tanzania na utawala mbovu chini ya CCM umemfilisi Mtanzania. Uwekezaji wa wazungu, kwenye mbuga za wanyama, hasa serengeti pia ni uhujumu.Ardhi iliyopewa na mahekari makubwa yote nchini kwa kipindi cha awamu uliopita ni kinyume cha sheria za ambazo zinekuwa kandamizi, Kama ardhi ni mali ya Watanzania , imekuwaje kutoa ardhi ya Watanzania bila kukaa kikao na wananchi hudika na kujadili maombi ya waliopewa ardhi. Badala yake mawaziri kama Tibainyuka, maraisi, na mawaziri kama nyinyi mliopewa kazi kusimamia mali ya watanzania mmewaza watanzania , mmewaibia, mmewadanganya, na mmekwenda kinyume cha sheria za nchi kutoa mali ya mtanzania kama mihogo kwa wazungu, wachina, waarabu ka mihogo, ambsyo naiiita hii mikataba ni batili. Hawa wsliopewa mikataba pia wanajua walivyowachezea nyinyi wasomi utata wanajua wazi. Ndo maana hawawaheshimu. Hamna usawa. Wapinzani waliililia katiba, sababu hata maraisi waliopewa kinga inabidi washtakiwe kwa makosa ya jinsi. Wamelia sana. Na watanzania ambao hawajaelimika bado sasa watauona ukwrli.Ni Africa tu watu na viongozi bado hawawathsmini watu wso, wsla mali zao.mikataba yotte ni wizi mtupu. Tanzania nchi Tajiri iliyopotoshwa na maraisi na mawaziri kama nyinyi mizigo msio na sifa kwa muda mrefu sana. Inabidi Tanzania irudie elimu ya uzalendo kwa vijana eote wsliosoma kwa kipindi cha miaka kumi na tano iliyopita sababu hawana uzalendo na elimu zao duni. Inabidi mikataba mokuu yote ipitiwe upya kwa kulikomboa Taifa. Uchaguzi ulipokonywa kuficha ukweli na kuogopa upinzani ungeingia ungefichua makubwa.
    Kunakitu kimemsukuma Muhongo aseme ukweli sasa sifshamu ni nini. Abanwe na aseme ukweli wa mambo yote anayoyajua ili Tanzania ijikomboe kwenye hili. Wizi wa mataifa makubwa kupitia wajinga nchi changa ndio huu. Ukoloni mambo leo ni hai. Ndo maana wanampiga vita sana Mugabe. Hajawaruhusu waibie Zimbwabwe tena. Ni raisi pekee mwenye utu na uelevu na kisomo cha hali ya juu kakataa kutumika na vibaraka. Mungu iepudhe Tanzania idije kuwa kama Iraq na nchi ya Gadafi, libya. Tunaenda huko tudipojiangalia.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad