Yafahamu Mambo Kumi Muhimu Kuhusu Ugonjwa wa Kisukari

Tarehe 07 Aprili 2016 ilikuwa ni siku ya Afya Duniani. Na kaulimbiu ya mwaka huu ilikuwa imelenga kupunguza ukuaji ya Ugonjwa wa kisukari. Taarifa zilizotolewa na shirika la afya (WHO) mwaka huu, jumla ya watu milioni 422 walikuwa wameathirika na Kisukari 2014. Kutokana na idadi hiyo kubwa shirika hilo lilieza mambo gani mtu anaweza kufanya kupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa huu.

Udaku Special tunakuwekea hapa mambo 10 yakuzingatia.

1.    Kila siku hakikisha kuwa umetembea hatua 10,000, punguza kula vyakula vya kusindika, hakikisha uzito wako ni sahihi, lala kwa saa 6 hadi 8 kwa siku, na pima kiwango cha sukari katika damu ukifikisha miaka 30 kama una ndugu yeyote mwenye Kisukari.

2.    Ulaji wa Nyama kwa kiwango kikubwa ni hatari kwa afya yetu. Hivyo punguza ulaji wa nyama hasa nyama nyekundu (Ng’ombe, Mbuzi)

3.    Kifungua kinywa ni mlo muhimu sana kwa afya ya mwili na akili kwani mwili hupata nguvu ya kufanya kazi kwa siku nzima. Kupata kifungua kinywa ni kitu muhimu sana kila mara kwani husaidia mmeng’enyo kufanya kazi kwa usahihi.

4.    Hakikisha mtoto anapata maziwa ya mama akiwa mdogo kwani maziwa ya mama yana kinga ya kumuwezesha mtoto kupambana na magonjwa. Huduma bora za hosipitali pia ni muhimu.

5.    Mshtuko wa Moyo huua watu wengi sana duniani. Watu 3 kati ya 10 duniani hufariki kwa sababu ya Mshtuko wa Moyo. Tunaweza kuzuia ugonjwa huu kwa kupata mlo kamili kila mara, mazoezi ya mwili na pia kuto vuta sigara.

6.    Takribani asilimia 10 ya watu wazima duniani wanaugonjwa wa Kisukari. Watu wenye kisukari wanahatari ya kupata magonjwa Moyo. Vifo vinavyosababishwa na Kisukari vimeongozeka tangu mwaka 2000, mwaka 2012 watu milioni 1.5 walifariki kurokana na Kisukari.

7.    Ulaji wa vyakula vyenye Sukari husababisha ugonjwa wa Kisukari. Mtu huugua Kisukari pindi mwili unaposhindwa kuzalisha Insulin kuishughuikia sukari kwenye damu. Kuto kufanya mazoezi, kuwa na uzito uliopitiliza kunakufanya kwenye hatari ya kuugua kisukari kadiri unavyoelekea uzeeni.

8.    Kiini cha yai hua na Cholestrol kubwa. Hivyo kama kiwango cha Cholestro mwilini kipo chini unashauri kula viini vya mayai mara kadhaa kw wiki.

9.    Kunywa maji ya kutosha kila siku, usisubiri hadi uwe na kiu ndipo unywe maji. Maji husaidia kuondoa sumu mwilini.

10.    Unashauriwa kula vyakula kama MTAMA; ambavyo huwa na Protein, Vitamins na madini kama Chuma, Calcium, Phosphorus na Pottasium, SAMAKI, VYAKULA JAMII YA KUNDE ambavyo huwa na Fibre na Protein, VIAZI VITAMU ambavyo huwa na Vitamin A na C ambayo husaidia kukuza kinga ya mwili.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad