Hii Ndiyo Tafsiri sahihi Ya Zawadi Katika Mahusiano Ya Kimapenzi

Mapenzi
Moja ya kitu ambacho huwa hakina kipaumbele sana katika mahusiano ya kimapenzi,  kitu ambacho kinachoitwa zawadi. Lakini ukweli ni kwamba zawadi ina maana kubwa sana katika mahusiano ya kimapenzi zaidi hata udhaniavyo.

Na Katika tafiti ambazo zimewahi fanywa ni kwamba, suala zima la utoaji zawadi katika mahusiano ya kimapenzi lilimekuwa likileta hisia zaidi katika upande mmoja. Yaani hapa nikiwa na maana ya kwamba jinsia ya kike ndiyo ambayo ipo katika kusubiri zawadi kutoka kwa jinsia ya kiume. Kutoka na suala hilo ndo maana watu wengi wamekuwa hawatilii maanani suala zima la zawadi. Lakini ukweli ni kwamba kila mtu anahusika kutoa zawadi.

Huenda ukawa bado nakuacha njia panda huelewi ni zawadi gani ambayo itampendeza mpenzi wako. Wala usipate tabu afisa Mipango nipo kwa ajili yako. Ipo hivi ili kujua zawadi ambayo mwezi wako anapendezwa nayo,  Unachotakiwa kukifanya ni kwamba kwa kuwa ni mpenzi wako ni mtu wa karibu jaribu kuchunguza ni kitu gani ambacho huwa anakipendelea sana,

Baada ya kupata majibu anza kufanya uchunguzi mwingine ni kitu ambacho huwa anapenda kulizungumzia sana,  baada ya kupata majibu, majibu hayo yaweke katika halmashauri yako ya kumbukumbu. Na mwisho wa siku mnunue kitu hicho kwani ndiyo zawadi itakayompendeza.

"Pia wakati mwingine maneno yangu sio sheria unaweza inanunua zawadi ambayo kiukweli unahisi fika itampendeza mwezi wako"

Hayo ni baadhi ya mambo machache ya kuzingatia katika kufanya uchaguzi wa zawadi ya kumpa mpenzi wako. Kwani zawadi ni ishara upendo imara. Pia imeshauriwa ya kwamba zawadi ni heri iwe ile ya kudumu kwani hii hukumbukwa daima.

Pasipo kupoteza muda tuendelee kidogo kwa kuangalia japo kwa uchache umuhimu wa zawadi katika mahusiano ya ndoa.

1.Huimarisha uhusiano na kuongezeka mapenzi ya kweli
Pindi utoapo zawadi kwa mwenzi wako,  mwenzi huyo hujihisi yeye ni wa thamani sana mbele yako.  kwani zawadi kutafsiriwa na mpokeaji kama ni mtu wa thamani sana,   mtu ambaye anapendwa kweli .   hivyo pindi ufanyapo kitendo cha utoaji wa zawadi yeyote ile kwa mwenzi wako, hufanya mahusiano yenu yaimarike na si kuteteleka.

2. Humfanya mtu ajihisi yupo mahali salama.
Usishangae huo ndio ukweli, kama ulikuwa hauna kawaida ya kumpa zawadi mpenzi wako basi anza kufanya hivyo mara moja.  Kwani zawadi hutafsiwa na mpokeaji ya kwamba yupo mahali sahihi. Hivyo ili kuweza kuudumisha upendo wako na mwenzi wako jenga utaratibu wa kumpa zawadi mpenzi wako.

3. Zawadi huacha kumbukumbu.
Hakuna kitu ambacho huacha alama kubwa katika mahusiano kama zawadi. Hivi hajawahi kukutana na mtu anamwambia ya kwamba kitu hiki alinipa fulani?  Bila shaka umewahi kukutana na mtu wa aina hiyo.  Kama ndivyo hivyo amini ya kwamba zawadi huacha alama katika mahusiano.

Na ili kuacha alama hiyo, kama nilivyosema hapo awali ua kwamba zawadi ni lazima iwe ni ya kudumu. Pia kabla sijaweka nukta nikumbushe pande zote mbili mvulana na msichana ana haki ya kutoa zawadi kwa mwezi wake. Hivyo nikusihi ya kwamba ujijengee utaratibu wa kutoa zawadi kwa mwezi wako
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad