Mabasi ya Mwendo Kasi ni Kichefuchefu...Nikki Mbishi Awashtaki Kwa Magufuli

Rappa, Niki Mbishi amemtaka Rais John Pombe Magufuli kutupia jicho katika mradi wa mabasi yaendayo kasi (DART) kwamba kama asipofanya hivyo kuna uwezekano mkubwa mradi huo ukafa bila kutimiza malengo yaliyokusudiwa.


Nikki anayetamba na 'hit' ya 'Dada pumzisha mwili wako' amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa twitter baada ya kuona mapungufu kutoka kwenye mradi huo ambapo ma -bus yamekuwa yakijaza idadi kubwa ya watu na kudai ni kupitiliza kiwango kilichokusudiwa.

"Hadhi ya mwendokasi ni 'level seat' siyo kushonana kama embe toka kibada Mzee Magufuli tazama hilo, mradi unakufa 'soon'. Mwendokasi watu wanajazana kama '3rd class train' ya India yatadumu kweli
?" aliandika Nikki Mbishi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad