Itatumia muda wa saa nne na nusu kutoka Mombasa hadi Jiji la Nairobi,, Awali wasafiri walikuwa wakitumia takriban saa 8 kwa njia ya basi,
Reli hiyo ina urefu wa kilomita 472 ambapo treni zitakuwa zikisafiri kwa kasi ya wastani ya kilomita 120 kwa saa na kutumia muda wa saa nne na nusu kutoka Mombasa hadi kufika Jiji la Nairobi, ikiwa ni safari ambayo ilikuwa ikitumia takriban saa 8 kwa njia ya basi.
Baadhi ya wananchi walioshuhudia uzinduzi huo wamesema treni hiyo itakuwa mkombozi kwao kwa madai kuwa hapo awali walikuwa wanapata shida kubwa katika kusafiri kutoka Mombasa hadi Nairobi.
"Hakika ni develepment ya maana sana kwa maana upande wa transport kitambo ilikuwa inachukua muda mwingi sana kwa gari kutoka Mombasa hadi Nairobi lakini hii nasikia inachukua masaa manne so itakuwa ni imetupeleka 'far with other developed courients" alisema Samuel Umma kutoka kaunti ya siaya