Acha Kulialia Umasikini..Hizi Hapa Aina ya Biashara Ambazo Unaweza Kuzifanya kwa Mtaji wa Kuanzia Elfu 10 Hadi 50..!!!


1,DAGAA WA BUKOBA
Dagaa hawa wanapatikana masoko mengi, hawa wanakua hawana mchanga kabisa, wanauzwa kg moja elfu nane huwa inashuka had elfu tano, hawa unanunua vifuko unapack unauza mtaani kifuko buku 

Kwenye kilo moja unaweza toa vifuko 15 sawa na elfu kumi na tano so elfu mbili vifuko elfu tano faida. Pia unaweza uza dagaa wa kigoma, zanzibar au mwanza waliokangwa

BIASHARA YA MATUNDA
Siku hzi watu wengi hasa maofisini wanapenda kula matunda andaa kwa usfi matund yako hapa unaweza tumia elfu kumi na tano, 

Unanunua matunda mchanganyiko tikiti, ndizi, tango, karoti, papai, parachichi matunda ya elfu kumi na tano buguruni au stereo ni mzigo nunua vifungashio vile vya kuwekea matunda pack matunda yako ambapo yakiuzika vyema unaondoka na faida nusu kwa nusu

JUICE ZA MATUNDA,
Matunda ya elfu kumi waweza toa had lita kumi za juice ambapo lita moja ni sawa na glass tano au nne za juice so kwenye lita kumi upata grass 40 sawa na elfu ishirin ukitoa matunda,sukar na vigras unafaida elfu tano,

BIASHARA YA MKAA
Gunia la elfu 30 unaweza kutoa mafungu 45 ya mkaa sawa na elfu arobain na tano faida elfu kumi na tano

MOBILE GENGE,(GENGE LINALOTEMBEA)
Watu wengi sasa hiv mna smartphone tangaza unauza nyanya, vitunguu karoti, na mazagazaga mengine ya jikoni, ukipata order unaenda ilala soko la wakulima unajumua vya kutosha unapeleka faida hapa ni nusu kwa nusu, pia unaweza tembezea majirani zako kutegemeanana sehemu unayoishi,

BIASHARA YA BITES
Hapa nazungumzia crips sambusa chapati maandazi mihogo ya kukaanga, vitumbua karanga za mayai, ubuyu, korosho, visheti etc unaweza sambaza vitafunwa maofisini as package kwamba pack moja ina andaz sambusa chapati na kachori au ukauzia nyumbani moja ya vitafunwa hivyo, Bites as wel peleka kwenye maduka na supermaket faida yake huwa nusu kwa nusu

BIASHARA YA VINYWAJI BARIDI STEND ZA DALADALA
Unaweza uza hata kwenye ndoo kama huna deli, nunua mabarafu nunua vinywaji tafuta kijana au wewe mwenyewe uza stend za daladala inalipa saaana

BIASHARA YA UJI WA ULEZI, UJI WA MCHELE NA MAKANDE
Kodi toroli jaza chupa zako uji aina hzo tembeza kwenye magereji na sehem za bodaboda unaweza tembeza mwenyewe au ukampa kijana faida ni mara mbili ya mtaji ukitumia elfu kumi jua itapata elfu 30

BIASHARA YA MBOGAMBOGA,
Unaweza funga kwenye pack mchicha tembele chinese ukatambeza kwa majirani na marafiki kama umetingwa unampa kijana ukauza mtandaoni unaoeleka kwa order ukatembea kwenye mahotel na migahawa kuomba uwauzie mboga mboga wewe unazifuata mabondeni unaenda kuuza town

BIASHARA YA KUKU VITUO VYA DALADALA
kuku wa kisasa mmoja elfu tano na kuku huyo kipande ni buu jero ina maana kwenye kuku mmoja unatoa elfu saba faida elfu mbili na kwa siku minimum unaweza uza kuku watano hadi kumi hukosi kurud na faida elfu kumi au elfu tano ukitoa mafuta na kuni

MNAOKAA USHUANI BIASHARA YA FIRIGISI,
njoo manzese nunua firigisi kawauzie wakishua pia unaweza tangaza kwa mitandao ukawa ubapokea order ya kusambaza firigisi(idea yangu hii) hahhahahah

Hizo ni baadhi ya biashara ndogondogo ambazo mtaji sio mkubwa ila ukizitilia maanani zinafaida saaana

Kinachotuangusha wanawake ni uthubutu wengi hatuna uthubutu tunafikiri biashara fulani ni ya watu fulani hapana hebu fanya kwa nia na umakini, kuwa na nidham ya pesa lazima utafanikiwa ,mimi nilikua nauza ice cream ubuyu,karanga na juice za kufunga na Mungu aliniona pakubwa (ipo siku ntatoa ushuhuda humu) 

Nilikua sister duu familia bora but sikuangalia hayo coz yote ni ya babangu mwisho wa siku lazima niwe na changu nikathubutu, SIJAWAHI KUFANYA BIASHARA YA MTAJI WA MAMILIONI NAFANYA HIZIHIZI NDOGO COZ NDIZO ZINAWAGUSA WATU WENYE HALI ZOTE , maandazi ya mama Ngina wananunua matajiri na wasio na kipato kikubwa , kisamvu cha mama ngina wananunua watu wa hali zote karanga za mama ngina wananunua watu wa hali zote unga ubuyu nk

NIDHAMU ya pesa. wengi wanaanguka kibiashara kutokana na kutokua na nidham ya pesa unatumia pesa nyingi kuliko unayoingiza, kuwa na Limiti ya matumizi faida unayoipata hata kama ni sh mia hamsin weka hamsini jilipe mshahara hap ndipo utapata hamsa ya biashara na biashara itakua usiwe muoga kuuliza kupita maofisini mtaani kutangaza biashara yako, 

watu wote wenye mafanikio waliweka aibu kando, kuna huyu dada zanana juice aliniinspire kwa kweli alianza biashara ya juice na mtaji wa elfu tano anatembeza mtaani na nimrembo haswa antembea na dumu la juice barabarani na degree yake kichwan hakuna aibu angalia now yuko wapi anamiliki bonge la juice bar ya kisasa mno so tujifunze kutoka kw waliofanikiwa sio lazima wote tuende china sio lazima wote tuwe na boutique do little things in a great way lazima utafanikiwa na ndio maana

Wengi hukata tamaa kufanya biashara watapata wapi wateja jaman saiv dunia ni kama kijiji mimi nipo dar but watu wa songea wanakula karanga zangu natuma maandazi arusha smart phone yko ndio duka lko no moja, phone book yako ndio watej wako, achna na magroup ya umbeya WhatsApp hkikisha unazungukwa na watu ambao mtafnya biashra utatangaza ubuyu watanunua, majirani kuzurul kila mtaa beba vipakti vya ubuyu uza karanga etc

Seminar za ujasiliamali huko ni muhimu zaid penda kuhudhulia semina utanue mawazo nanuoatemawazo mapya na nhuvu ya kuifnza kutoka kwa waliofanikiwa

mali bila daftar huisha bila habar hakikisha unaandika kila pesa unayotumia ili mwisho wa siku uweze kujua unapigaje hatua.

Chanzo JF

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nimependezwa sana na mada hizi lakini tuwe tunajulishwa tahadhari gani zichukuliwe ili kuboresha au kufanya biashara izidi kusonga mbele

    ReplyDelete
  2. Daah umenikosha nakujiona Mimi Ni jasiri mno je nakwama wapi halafu mazingira yote Ni chanya, naomba niwambie ntakupataje kwa ushauri zaidi. Ahsante

    ReplyDelete
  3. Mimi nataka kufanya biashala ya samaki sasa sierewi bado

    ReplyDelete
  4. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad