Askari Wawili wa Usalama Barabarani Wauawa Kwa Kupigwa Risasi Kibiti

Picha imefichwa kwa Maadili
Rufiji. Askari Polisi wawili wa kikosi cha usalama wa barabarani wilayani Kibiti ambao majina yao bado hayajatambulika wapigwa risasi na watu wasiojulikana katika Kijiji cha Msafiri,Kata ya Bungu wakiwa kazini.

Mbali na kupigwa risasi, pia watu hao wamechoma moto gari moja na pikipiki moja za askari hao kisha kutokomea kusikojulikana.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Onesmo Lyanga amethibitisha kutokea kwa tukio na kusema anafuatilia.

Tukio hilo limetokea kilomita chache kutoka eneo ambalo waliuawa askari polisi wanane kwa kupigwa risasi katika eneo la Mkengeni walipokuwa wakitoka doria katika Kijiji cha Jaribu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad