Nimesoma hotuba ya bajeti kurasa zote kuanzia ukurasa wa kwanza mpaka wa mwisho hakuna chochote kilichozungumzwa kuhusu maslahi ya mfanyakazi wa umma hususani mshahara wa mtendaji huyu wa serikali.
Licha ya matambo na mbwembwe nyingi katika uwasilishaji lakini serikali imeshindwa hata kutaja kima cha chini tu cha mshahara!Imeshindwa hata kusema tu maneno machache ''tumezingatia maslahi ya mtumishi katika bajeti hii''
Hii serikali toka iingie madarakani imekuwa na mazoezi kandamizi tu kwa mfanyakazi, watumishi hewa, vyeti feki, lawama za kila aina lakini imekuwa jeuri kuhusu kuzingatia maslahi ya wafanyakazi hawa.
Wabunge tunawaomba msimamie na kupigia kelele suala hili katika mjadala wa bajeti.
Chanzo JF