Bakita Yatema Cheche na Kusema Katika Kiswahili Hakuna Neno Makinikia Bali Neno Sahihi Ni....!!!


Akizungumza exclusively kabisa mmoja wa Viongozi wa juu la Baraza la Kiswahli Tanzania ( BAKITA ) jina kapuni amesikitishwa sana na kitendo wa Wajumbe wa Tume ya Kuchunguza mchanga wa Madini kuliibua neno la uwongo na hadi kumdanganya Mheshimiwa Rais na Watanzania kuwa neno sahihi la ule mchanga ni Makinikia wakati neno sahihi ni Mashobo.

Kiongozi huyo ameenda mbele na kusema kuwa sasa wamesamehe Watu hao wa hiyo Tume japo wanajipanga kwenda kuonana nao ili wawaambie walirekebishe hilo neno katika maelezo yao na pia ameviomba Vyombo vya Habari vyote nchini kuacha tabia ya kukurupuka kulitangaza au kuliandika neno pasipo kuonana na wao BAKITA kama wanalitilia shaka kwani umefanyika upotoshaji mkubwa juu ya hili neno Makinikia. 

Haya Watanzania wenzangu kuanzia sasa tuachane na neno Makinikia badala yake tuanze kulizoea neno ambalo ndilo sahihi na hata wenye Kiswahili chao Watu wa BAKITA wamelithibitisha kuwa ni la Mashobo narudia tena kwa msititizo siyo Makinikia bali ni Mashobo.

Naomba kuwasilisha na kila la kheri nyote.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad