Toka juzi baada ya Magufuli kukutana na CEO wa Barick vyombo karibu vyote vya habari vimejaa 'habari za pongezi' kwa Rais kwa 'kuweza kufanikisha kulipwa' tulichokuwa tunaidai hiyo kampuni.
Taarifa za habari za TV karibu zote na magazeti habari ni hizo hizo.
Licha ya ukweli kuwa jana hiyo hiyo Barrick na ACACIA wote wametoa taarifa za kukataa kulipa chochote sisi vyombo vyetu ni kama hiyo taarifa 'haituhusu' kabisa tuko bize na pongezi.
Inanikumbusha wakati wa Babu wa Loliondo jinsi ambavyo media zoote zilivyokuwa zinaripoti 'miujiza' ya babu huyo huku zikiwa hazitaki kabisa kuripoti taarifa za wagonjwa waliokuwa wanakufa baada ya kutoka huko Loliondo.
Hata taarifa za wataalam wa nje waliofika na kusema 'hakuna tiba' huko Loliondo wagonjwa wasiache dozi za hospitali zilipuuzwa.
Tulikuwa nchi nzima tuko excited na babu wa Loliondo na kikombe chake.
Yeyote aliongea vingine alionekana 'msaliti' na sio 'mzalendo'
Wapo waliotaka Babu wa Loliondo apewe tuzo maalum na kadhalika na kadhalika.
Vyombo vyetu vya habari ndo viligeuza habari ya 'kuuza' na kuwajaza watu ujinga uliopelekea hata watu wengine kupoteza maisha la kusikitisha hii tabia haijawahi kukemewa.
Sasa tuko na kupongezana na kuambiana uwongo mtupu licha ya wahusika kutoa ukweli wao kuwa hakuna walichokubaliana kulipa sisi ndo kwanza na wengine wanataka tuzo kwa tume na Rais aongezewe muda kwa 'haya mafanikio ambayo siyo ya kawaida'.
Chanzo JF