=> Kiwango cha ukuaji uchumi 2016/2017kimeendelea kukua kwa wastani wa asilimia saba ikiwa ni pungufu kidogo ya kile kilichotarajiwa awali. Makadirio ya awali yalionyesha kuwa uchumi huo ungekua kwa wastani wa asilimia 7.2.
=> Hali ya ukuaji uchumi imeendelea kushuhudiwa katika kiwango kilekile cha awali cha asilimia saba na hii imechangiwa na mambo mengi ikiwamo baadhi ya sekta kutofanya vizuri. Sababu hizo ni pamoja na kushuka wa sekta ya kilimo iliyotarajiwa kukua kwa asilimia 2.9, lakini malengo hayo hayakufikiwa na badala yake yalikuwa kwa asilimia 2.1.
=> Sekta ya biashara ilikuwa 6.7% hali ambayo ni tofauti na makadirio yaliyowekwa awali yaliyokuwa 7.8%
=> Eneo la chakula limechangia kufikia kwa malengo ya ukuaji uchumi. Makadirio yetu yalikuwa kwamba sekta ya chakula ingekua kwa 8%, lakini bahati mbaya ilishuka na kuwa 3.7%.
=> Kuna sekta zimefanya vizuri na kusaidia uchumi wa Taifa, sekta hizo ni pamoja na habari na mawasiliano, madini na kiashirio cha kuendelea kukua kwa sekta ya viwanda.
=> Kwa mwaka 2016/2017 Serikali ilipanga kutumia Shilingi Bilioni 11,820.5 kwa ajili ya bajeti ya mandeleo. Hadi April 2017 fedha zilizokuwa zimetolewa ni Shilingi Bilioni 4516.7 sawa na Asilimia "38" ya Bajeti nzima.
2017/2018
=> Serikali imetenga bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2017/18 kwa ajili ya kufufua kiwanda cha matairi yaani General tyre.
=> Serikali inafanya utaratibu katika kuboresha maisha ya wananchi na watumishi wa umma kwa kuweka malengo na bajeti katika kutekeleza hayo.