CCM inahitaji Upinzani Mpya, Huu wa Sasa ni Upinzani Chakavu na Uliozeeka


Chama tawala cha CCM ni chama ambacho kimepita katika safari ndefu sana mpaka kufikia hapa kilipo leo.Safari hiyo imekua ya furaha huzuni , machozi na jasho.

Katika miaka yote imekua ikikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa vyama vingine vya siasa (Wapinzani) hususani katika uchaguzi lakini mara zote imekua inaibuka na ushindi wa kishindo katika kila uchaguzi.
Mathalani mwaka 1995 tulishuhudia upinzani mkali ambao mpaka leo haujapata kutokea tena.

Lakini leo mambo yamebadilika,upinzani ule ninaoujua mimi haupo tena , upinzani ule ulioweza kutingisha nchi umetoweka , upinzani ulioweza kulitikisa bunge la Jamhuri na kung'oa mawaziri umeyeyuka mithiili ya barafu kwenye jua.
Aina ya upinzani tulio nao sasa ni mwepesi sana kuwahi kutokea .

Madhara ya CCM kufanya mageuzi makubwa katika taasisi hiyo chini ya falsafa ya "CCM MPYA NA TANZANIA MPYA" yameanza kuonekana katika vyama vyote vya upinzani Tanzania.
Upinzani umekosa mashiko na hoja mujarab kutokana na kasi ya CCM MPYA katika kuisimamia serikali kutekeleza kwa vitendo Ilani ya mwaka 2015.

Ajenda kubwa ambayo walikua wanaitumia sana wapinzani ilikua ni ajenda ya ufisadi na hii ndio ilikua kete yao pekee iliyokua inawapa umaarufu.Lakini tokea serikali hii ya awamu ya 5 iingie madarakani ni kama vile vyama hivyo vimepigwa ganzi, havisikiki tena vikizungumzia ufisadi, na hii ni kwa sababu kuu mbili.

1.Uamuzi wao wa kumchukua ndugu Edward Lowassa kua mgombea urais umewafunga midomo kabisa kuzungumzia sakata la ufisadi maana kila Mtanzania anakumbuka miaka ya nyuma jinsi chadema kilivyokua kinazunguka nchi mzima kwa magari na helkopta kumtangaza Lowassa kua ni fisadi mkubwa (Fisadi nyangumi) na sehemu pekee anayostahili kuishi ni gerezani tu.
Leo hii wapo naye wanakunywa chai pamoja.

2.Kasi ya Mh Rais Magufuli katika kushughulika na wala rushwa na mafisadi.
Hatua ya ujenzi wa mahakama ya mafisadi ,utumbuaji na ukamataji wa watuhumiwa wa vitendo vya rushwa na ufisadi (Mf.Escrow Scandal) vimewatia ubaridi wapinzani hawa kuongelea tena kwa sababu kazi nzuri inafanyika ya kudhibiti na kufuta kabisa rushwa na ufisadi.Wamekosa points za kuongelea katika muktadha huo.

Serikali ya awamu ya 5 imefanya mambo makubwa na mazuri sana tangu iingie madarakani na tena mambo hayo yamefanywa kwa namna bora zaidi kupita matarajio ya wengi wakiwamo wapinzani ambao hawakutegemea kama yatafanyika. Mambo hayo yameleta tija na kufufua matumaini mapya kwa wananchi na Taifa zima.

Serikali inafanya mambo hayo kwa umakini mkubwa kuhakikisha haifanyi makosa na ndio maana kila wapinzani wakijaribu kuchungulia kuona labda wataona makosa wanaambulia patupu , wanaishia katika kuzusha uwongo usiwaosaidia wananchi na tena usio na hata lepe la ukweli.

Matokeo yake ni kwamba hoja zao za kitoto zinakosa ladha kwenye masikio ya wananchi zinadumu kwa kipindi kifupi sana kisha zinatoweka.

Ni wazi dhahiri kwamba upinzani wa Tanzania unatereka na umeshazeeka , na CCM inahitaji ladha mpya ya upinzani utakaotoka kwenye chama kipya kabisa.
Upinzani huu sasa uliojielekeza katika kusaliti rasrimali za taifa lao na kuwatetea mabwanyenye, wanyonyaji na makabaila wa kizungu umefikia hitimisho lake.
Upinzani huu uliofikia hatua ya kupinga hata yale mambo (Issues) ambayo walikua wanayapigia kelele kwa miaka mingi ni upinzani mzee.

Uzee na uchakavu wa vyama vya upinzani umeonekana pia katika chaguzi za marudio hivi karibuni , ambapo katika nafasi za madiwani,wenyeviti wa mitaa, vitongoji na vijiji ambapo kwa ujumla yake Chama Cha Mapinduzi kimeshinda kwa zaidi ya asilimia 99%.
Pia kasi kubwa ya viongozi na wanachama wa vyama hivyo kujiunga na Chama Cha Mapinduzi ni mfano mwingine wa uzee na uchakavu wa upinzani vya Tanzania kwa mfano tumeshudia madiwani kutoka kule Wilayani Arumeru Mkoani Arusha na mikoa mingine wakikihama chama hicho na kujiunga na CCM achilia mbali aliyekua Makamu Mwenyekiti (Taifa,) wa chadema Said Arfi ni ishara mojawapo kwamba CCM MPYA imekidhi matarajio mengi ya wananchi wakiwamo hao wapinzani walioamua kwa hiari yao kurudi CCM na kumuunga mkono Rais Mh. Dr John Pombe Magufuli.

CCM MPYA ya sasa imejizatiti katika masuala mazima ya uadilifu, uaminifu, uwajibikaji,weledi, uchapakazi na kujishughulisha kutatua kero za wanyonge wa Tanzania.Pia CCM ina maono mapana katika kujenga chama bora kitakachozaa serikali bora na ndio maana iko mbioni kuanzisha chuo cha kuandaa viongozi wa hapo baadae.Hii ni tofauti na vya upinzani

Miaka 25 ya mfumo wa vyama vingi vya siasa vyama hivyo vimeshindwa kuandaa viongozi wake.
Vyama huokoteza okoteza watu wasio waadilifu na weledi au kusubiria rehema za makada wa CCM waliokengeuka na kujiunga na vyama hivyo ambao huwapachika katika nafasi za uongozi ambao mwisho wa siku huishia kuharibu mambo.
Upinzani unaoshindwa kuandaa viongozi katika miaka yote hiyo ni upinzani usio makini ,chakavu na mzee.

Kasi ya CCM MPYA chini ya Serikali adilifu na imara ya Mh Dr .Magufuli imefifisha uwezo wa kujenga hoja wa wapinzani,imekata miguu waliyokua wanatumia wapinzani kusimamamia na kubwa zaidi imezeesha vyama vya upinzani kwa kutekeleza Ilani ya CCM2015-2020 kwa spidi kubwa na ya ajabu.

Ile kauli ya Mh Rais ya kwamba mpaka kufikia mwaka 2020 vyama vya upinzani vitakua vimejifuta vyenyewe, inaenda kutimia.

Upinzani huu uliokosa msimamo,uadilifu, uaminifu, uwajibikaji ,weledi na maono umeshazeeka tunahitaji kuundwa kwa vyama kipya vitakavyotoa changamoto kwa CCM ,lakini chadema cuf, nccr ni muda wao wa kupumzika siasa kwa kua vimeshazeeka kihoja, kimkakati na kisera.

Vijana wote walio katika vyama hivyo au wanaotarakia kujiunga na vyama hivyo hawana tofauti na watu waliopanda boti iliyotoboka boriti kwani muda wowote itazama.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ni kweli kabisa vyama vya upinzani havina jipya kwa sasa, watabaki ku'badilisha gia angani kila baada ya miaka mi'5......CCM woyeeeee......HAPA KAZI TU!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad