KATIBU wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Humphrey Polepole amesema viongozi na watendaji watakaoitumia CCM kwa faida yao binafsi siku zao zitahesabika.
Aidha, Polepole alisema chama hicho kitaendelea kuwa imara na daraja kati ya wananchi na serikali yao ili kuhakikisha kinawasemea watu wengi, maskini na wanyonge ambao haki zao zimeporwa na kupokwa kwa muda mrefu.
Akihutubia mkutano wa ndani wa viongozi wa matawi na kata wa chama hicho waliochaguliwa karibuni, katibu mwenezi huyo aliwataka viongozi na watendaji ndani ya chama hicho kuacha kukitumia kwa faida yao binafsi bali watangulize mbele maslahi ya wengi, vinginevyo siku zao zitahesabika.
Katibu huo alikuwa akizungumza na mabalozi na viongozi wa CCM ngazi ya wilaya na mkoa akiwa katika ziara ya mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Ziara hiyo ina lengo la kumpongeza Rais John Magufuli kwa utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2015 hadi 2025 pamoja na kuimarisha uhai wa chama hicho.
“Viongozi wasio waadilifu ndani ya Chama watambue huu ni wakati mwingine... waanze kubadilika," alisema Polepole "maana hatutowavumilia watu wanaotumia mali za chama chetu kwa manufaa yao."
"Watambue siku zao zinahesabika... wale wote walio na makandokando ya uovu wasipate nafasi ya kupata uongozi wowote ndani ya chama.
"Tunawatafutia engo ya kula vichwa vyao.”
Aidha Polepole alimpongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri anazozifanya.
Naye katibu wa CCM mkoa wa Mwanza, Raymond Mwangwala alikemea mnyukano miongoni mwa watendaji wa serikali na viongozi wa kisiasa waliomo kwenye vyombo vya dola unaofukuta katika baadhi ya halmashauri mkoani Mwanza.
“Kuna shida katika baadhi ya watumishi walioaminiwa