Leo akizungumza na wanahabari, Dkt. Mashinji amesema kwamba kuna umuhimu mkubwa wa katiba ya Jaji Warioba kuanza kudaiwa maana itakuwa suluhisho la kudumu kuepusha matokeo ya wizi wa rasilimali serikalini kutokana na mapendekezo ya wananchi yaliyowekwa.
Dkt Mashinji amesema kuwa mikataba mibovu inayopitishwa na wabunge haitokuwepo tena bungeni kwa kuwa katiba itakuwa inawabana kuwajibika kwa ufasaha la sivyo watawajibishwa na wananchi waliowapa dhamana ya uwakilishi.
"Ile Katiba ya Jaji Warioba ndiyo inatakiwa sasa hivi wananchi tuanze kumuomba Mh. Rais atupatie kwa sababu hata hii mikataba mibovu inayopitishwa ni kwa sababu wabunge wanafanya kazi kwa ushabiki. Ila kwa katiba ya Warioba watu watawajibika maana watajua wakiharibu wananchi watawawajibisha hata yale makofi yatapungua, na wabumge wataongeza ufanisi na uwajibikaji" alisema Dkt Mashinji.