Chadema Watoa Tamko Juu ya Mnyika Kusukumwa na Askari wa Bunge...!!!


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Ubungo kimesema kitendo cha Mbunge wa Jimbo la Kibamba, John Mnyika kutolewa kwa nguvu Bungeni Juni 2, si cha kiungwana.

Akizungumza leo (Jumapili), Juni 4,  Katibu Mwenezi wa Chadema, Ubungo, Perfect Mwasiwelwa amesema Wapinzani akiwamo na Mnyika wamekuwa watetezi wa masuala ya madini kwa miaka takribani 20 ila sasa wanaonekana sio wazalendo wa Taifa lao.

"Kitendo cha Mnyika kubebwa mzobemzobe na kutupwa nje ya mlango wa bunge na ukiangalia mazingira alitaka kudondoka, kwa kweli ni kitendo cha kinyama, sio cha kiungwana, sio cha kibinadamu na Kitanzania kabisa," amesema Mwasiwelwa.

Amesema kuwa Chadema inapinga matumizi ya nguvu  kwa ajili ya kuzima upinzani kupigania suala la madini kama ilivyofanyika kwa Mnyika ambaye ni Waziri kivuli wa Wizara ya Nishati na Madini.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hao nao sifa ndio zinazowaponza, kwani angekaa kimya asingekuwa rijali......hovyoo.....kavuna alichokipanda

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad