Cheen Beenz na Chuki Binafsi Kwa Navykenzo na Wasanii wa The Industry


Huyu msanii anayejiita Cheen Beez kila mara amekuwa akiojiwa na media tofauti akilalamika kuwa amewatungia Baadhi ya nyimbo Navykenzo na Wasanii wao Rosa ree na Vanessa Mdee na kuonyesha uchungu kuwa wanapiga hela ndefu kwa ajili yake.....

Ki ukweli mie hii hainingii akilini hata kama kweli aliwatungia hizo baadhi alizodai , kila mtu anajua Uwezo na Navykenzo, Vanessa Mdee na Rosa Ree wasanii anaodai aliwatungia viitikio alivyokuwa katika lebo hiyo....

Hawa wasanii ukiangalia tu kwa haraka haraka wanauwezo kuliko yeye na wanahit songs nyingi hata before yeye hajajulikana katika game ya music, nachoona kwake ni chuki binafsi alizonazo kutokana na mafanikio wanayopata kila siku zinavyoenda huku yeye akizidi kupiga jalamba na nyimbo zake ambazo hazieleweki huku akidai anauwezo mkubwa wa kutunga nyimbo..

Namshauri tu akae kimya kwani hizo ni kiki hewa tuu huku anaowashutumu hawana hata time ya kumjibu ...

Atumie huo uwezo wake kujitoa kwanza yeye mwenyewe naye apige hela kibao....la sivyo namtabiria hata hiyo lebo ya wanene siku si nyingi watampiga chini kwa kutoona mafanikio yake bali longo longo na kujidai tu

By Laikon

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad