Ukweli Mchungu..Kama JK na Mkapa Hawaguswi..Kisheri Chenge na Genge Lake Pia Hawastahili Kuguswa,na Wkienda Mahakamani Wanaweza Kujitetea kwa Njia Hizi..

Andrew Chenge

Mahakama huendeshwa na doctrine au itikadi ya haki bila upendeleo.

Kauli tata za Magufuli na Ndugai za kuwakingia watuhumiwa nambari moja ufisadi wa Madini akina Mkapa na JK ni utetezi tosha kwa Muhongo, Karamagi, Yona na Ngeleja.

Watakapowapeleka mahakamani mawaziri wa zamani wa Madini watakuwa na utetezi wa aina tano:-

1) Moja, "collective responsibility" yaani uwajibikaji wa pamoja katika baraza la mawaziri kwa hiyo hawawezi kutolewa kafara kwa kutekeleza maamuzi ya baraza la mawaziri.

Mahakama itawaachia huru kwa sababu tu wamebaguliwa na haki zao za kikatiba za kutendewa sawa na wajumbe wote wa baraza la mawaziri hususani wenyeviti wa vikao hivyo ambao ni Mkapa na JK. Utetezi huu unaitwa "misjoinder of the accused".


2) Kutomshtaki JK wakati alipokuwa waziri wa Mambo ya Nje miaka ya 1997-2000 wakati mikataba ya Bulyanhulu na mingineo ilisainiwa baada ya kupitishwa na baraza la mawaziri na hakuwa na kinga ya Urais kwenye vipindi tajwa na kutomshtaki ni kuwabagua mawaziri walioshtakiwa na utetezi wa " misjoinder of the accused" ni haki yao na lazima wapewe kwa kuachiwa huru.

3) Sheria ya wawekezaji ya mwaka 1997, sheria ya madini ya 1998 na hata ya 2010, sheria za kodi kuanzia 1998-2004 zilirandana na sera ya CCM ya kuvutia wawekezaji. Wao kwa kusaini mikataba husika walikuwa wakitekeleza sheria na misamaha walioitoa ni kuharakisha kasi ya kuwavutia wawekezaji.

Utetezi hapo ni kuwa hakuna jinai katika kutekeleza sera na sheria za nchi. Hakuna mahakama itawatia hatiani kwa hili.

4) Kauli zembe za Magufuli na Ndugai zinaingilia uhuru wa DCI, DPP, TAKUKURU na Mahakama kwa kuwasafisha watuhumiwa wakuu wa ufisadi ambao ni Mkapa na JK huku watuhumiwa Muhongo na wenzie wakitajwa na taarifa za kamati zilizoundwa na Rais kukidhi kiu za kisiasa na kuwatoa watuhumiwa tajwa kama makafara ya kisiasa haiwezekani vyombo vya utoaji haki kama mahakama viwatendee haki.

Kwa kuhukumiwa kwenye majukwaa ya kisiasa ni dhahiri tayari wamedhulumiwa haki zao za kujitetea kwa sababu Rais Magufuli na Spika Ndugai wameingilia uhuru wa mahakama.

Utetezi huu ni mzito wa watuhumiwa haki zao za kikatiba zimekiukwa pale mihimili miwili ya dola ambayo ni serikali na Bunge imeingilia uhuru wa muhimili mwingine wa mahakama katika kutoa haki.

Huu ni utetezi tosha wa kuwafutia mashitaka feki yenye msukumo wa kumjenga Magufuli na CCM yake kwa kupitia migongo dhaifu ya watuhumiwa.

Mahakama haitachelea kulinda uhuru wake kwa kufuta mashitaka ya kubambikiziwa.

5) Hakuna makosa yoyote ya kupokea rushwa ambayo wametuhumiwa kwa hiyo Mahakama haina jinsi bali kuwaachia tu. Makosa tajwa yangelidhoofisha utetezi wao kwenye namba 1-4 hapo juu kwa kubainika wajumbe wa baraza la mawaziri ambao hawajashtakiwa hawana makosa binafsi ya jinai. Hivyo, hawajabaguliwa.

USHAURI

Kama Mkapa na JK ni "untouchables" then their sidekicks are also the "untouchables"

Chanzo JF

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad