Mshambuliji wa Chelsea, Diego Costa amesema ametumiwa ujumbe mfupi wa simu kutoka kwa kocha Antonio Conte akitakiwa kutafuta maisha sehemu nyingine.
Ndoto za Costa kubaki kwenye Uwanja wa Stamford Bride zimezimwa na kauli hiyo ya kocha ambaye hivi sasa yupo kwenye harakati za usajili kwa ajili ya kukisuka kikosi chake.
Taarifa za mchezaji huyo kuondoka kwenye klabu hiyo mabingwa wa England msimu ulioisha, ziliaanza kuripotiwa kwenye vyombo vya habari kabla hata ligi hiyo kumalizika.
Costa alikuwa anahusishwa kuhamia Ligi Kuu ya China hata hivyo hivi karibuni alibadili mawazo na kutanga kwamba angependa kuendelea kubaki England.
Nafasi yake kubaki Chelsea imekuwa ndoto kutokana na uongozi huo kuongeza kasi kumsajili mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku.
Mchezaji huyo mwenye miaka 28 amepewa taarifa za kutokuwapo kwenye mipango ya Conte jambo lililomfanya kuiwa njiapanda.
“Nimetumiwa ujumbe mfupi kwenye simu kutoka kwa Conte akisema sipo kwenye hesabu zake za msimu ujao” alisema Costa alipokuwa akizungumza na waaandishi wa habari wakati timu yake ya Hispania ilipotoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Colombia jana Jumatano.
Costa alisema huenda kocha wake amechukua uamuzi huo kutokana na kufanyua vibaya msimu uliopita