Wakati nikiwa mdogo niliwahi kusikia wakubwa wangu wakisema ya kwamba mazoea yana tabu, kwa kipindi kile sikujua walikuwa wanamaanisha nini, ila kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo ninavyozidi kuelewa walikuwa wanamaniisha nini.
Nilichokuja kukigundua juu ya msemo huu ni kwamba mawazo ya binadamu ni mawazo ya mgando, naweza nikasema hivyo kwa sababu akili zetu tumezielekeza katika kufanya mambo katika mazoea. Kama mtu amezoea kula ugali muda wa mchana basi mtu huyo ukimpa wali muda wa mchana basi utamsikia mtu huyo akisema kwa kweli mimi kula wali mchana zijazoea.
Kwa mfano huo, angalia watu ambao wanafanya biashara fulani ambazo hazilipi, ukimwambia wafanyabiashara hao wafanye biashara nyingine watakwambia ya kwamba hawawezi kufanya biashra ambayo hawaijaizoea. Kwa majibu ya aina hiyo ndipo nianapokubaliana na usemi ule usemao ya kwamba mazoea yana tabu, hii ni kwa sababu watu wengi tunashindwa kufanya vitu vingine tofauti na tulivyovizoea.
Lakini kama kweli unataka mafanikio ya kweli ni vyema kwa jambo lolote ambalo unalifanya acha mara moja tabia kufanya vitu kwa mazoea kwani mazoea ni dalili za uvivu, unashangaa huo ndio ukweli ambao upo wazi. Hivyo kwa kila jambo ambalo unalifanya hakikisha ya kwamba unatafuta mbinu nyingine za kuweza kuwa bora zaidi.
Lakini pia unashauriwa ya kwamba Ili kufikia mafanikio zaidi ya hapo ulipo, ipo haja na ulazima wa wewe kujituma na kufanya kazi kwa bidii sana nje ya yale mazoea uliyojiwekea. Kwa mfano, kama umezoea kufanya kazi kwa saa 8, ongeza masaa mengine manne ya ziada. Kama umezoea kuamka sa 12, anza kuamka saa 11 alfajiri. Fanya kitu ambacho kitakutoa nje ya mazoea yako yaani ‘comfort zone’. Kwa chochote kile unachokifanya, fanya nje ya mazoea yako.
Hivyo kila dakika na kila sekunde, kama kweli unataka kuondoka katika hali uliyopo kwa sasa unachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kuachana mara moja ile tabia ya kuishi katika misingi ya kimazoea (comfort zone) ambayo umeyazoea, na kufanya hivi itakusaidia sana kujenga misuri mikubwa ya kukuwezesha kufika mbali zaidi kimafanikio.
Endapo utandokana na hali ya kufanya vitu kwa mazoea tegemea kupata mambo makubwa ya fuatayo;
1 1. Utapata mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi, hii ni kwa sababu utaongeza uwezo na muda wako wa kufanya kazi.
2. Lakini pia kama utaondokana na ile tabia ya kufanya kazi kwa mazoea basi jiandae kuwa mtaalamu kwa jambo ulifanyalo.
Hivyo tumalize kwa kusema ya kwamba unatakiwa kuachana mara moja tabia yako ya kufanya vitu kwa mazoe.
Tukushuru sana kila wakati kwa kuwa sehemu ya mafundisho haya kila siku, endelea pia kuwashirikisha wengine.
Imeandikwa na uongozi wa mtandao wa dira ya mafanikio,
Imani Ngwangwalu & Benson Chonya,
0713 04 80 35, 0652 015 024,
dirayamafanikio@gmail.com,
bensonchonya23@gmail.com,