Kufuatia kauli ya Mbongo Fleva, Baby Joseph Madaha maarufu kama Baby Madaha, aliyoitoa hivi karibuni kwamba ma-video queen wanaojaribu kuimba ndiyo wanaharibu heshima ya Muziki wa Kizazi Kipya, baadhi yao wameibuka na kumlipua vilivyo mwanadada huyo.
Bila kuwataja majina, Baby Madaha alisema kwamba wauza sura kwenye video mbalimbali za wanamuziki wa Bongo Fleva, ambao wanaingia kwenye muziki kwa mgongo huo, wanaharibu
muziki ambao wao wameujenga kwa muda mrefu.
“Ma-video queen wanaoingia kwenye muziki ilimradi tu, ndiyo wanaotuharibia huu muziki ambao tumehangaika na kuhaso nao kwa muda mrefu, kwa sababu wao wanaingia tu kirahisi ilimradi wanajifunza jinsi ya kuimba basi bila kujua kwamba kuna watu tumepata nao shida,” alisema Baby Madaha.
Kutokana na kauli hiyo warembo ambao wanafanya u-video queen huku wakiwa ni wanamuziki pia wamemjia juu Baby
Madaha na kumtolea maneno makali huku wakimtaka awe na heshima.
Warembo waliokerwa na kauli hiyo ni Amber Lulu, Lulu Diva na Gigy Money ambapo mapovu yao waliyatoa kama ifuatavyo;
AMBER LULU
“Huyo Baby M a daha ni mshamba, ameshachoka hana kitu kipya kwenye muziki, siyo mbunifu kwa hiyo wivu wa kuona vipaji vipya na wasichana wazuri kama sisi Amber Lulu, Gigy Money na Lulu Diva ambao tumepitia video queen. tulimkuta kwenye gemu na tumempita, Baby Madaha ni ‘very cheap’ kwa kweli.”
“Kwanza huyo Baby Madaha simfahamu vizuri na ningekuwa mimi ndiye yeye nimetokea BSS, ungekuta sasa hivi niko staa mkubwa Afrika lakini kwa kuwa hajiongezi ndiyo maana yupo hivyo alivyo, atuambie ana nyimbo gani inayovuma sana au amefanya kitu gani kwenye muziki ambacho tunakiharibu? Aache dharau maana hata yeye anadanga tu kwenye muziki.”
LULU DIVA
“Huo ni mtazamo wake, kwanza simfahamu Baby Madaha hivyo nashindwa kumzungumzia sana, ila angetuambia kitu gani cha maana alichokifanya kwenye tasnia ya muziki, video queen ni kazi kama nyingine ila watu wamekuwa wakiidharau tu.
“Nilifanya kazi hiyo kama daraja la kuniwezesha kufikia malengo ya kuwa mwanamuziki na nimefanikiwa kwa hilo, hivyo Baby Madaha anatakiwa kuangalia upya muziki wake yaani ni wapi alipokosea ili aparekebishe na siyo kusingizia watu.”
GLADNESS MALLYA, RISASI MCHANGANYIKO