Habari ya Uongo ya TBC iliyomhusisha Rais Magufuli yatua Bungeni

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe amesema Serikali ilichukua hatua stahiki za kinidhamu dhidi ya watangazaji wa kituo cha runinga cha TBC waliorusha habari ya uongo iliyomhusisha Rais Trump wa Marekani akidaiwa amemsifia Rais Magufuli.



Waziri Mwakyembe ametoa kauli hiyo leo, Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi aliyetaka kujua Serikali ilichukua hatua gani juu wa Watangazaji waliosoma habari hiyo huku akidai kuwa bado anawaona katika kituo hicho cha runinga.

“Tulichukua hatua za kinidhamu kwa kosa ambapo kila binadamu hapa duniani anaweza kulifanya, yametokea matatizo kama hayo hayo Kenya yamefanyika watangaji wamerudi, na sisi tulichokifanya kuchukua hatua ya muda mfupi ili wawe waangalifu zaidi ni kitu kinafanyika kila siku leo, Mwenyekiti nikikuletea mfano wa Magazeti yanayochapishwa kila siku nakuhakikishia asilimia 60 ndani kuna makosa kwahiyo ni makosa ya kibinadamu,”

Waliosimamishwa kazi kwa kipindi hicho ni pamoja na mtangazaji aliyeisoma habari hiyo, Gabriel Zakaria na wengine ni Elizabeth Mramba, Prudence Constantine, Dorothy Mmari, Ramadhan Mpenda, Leya Mushi, Alpha Wawa, Chunga Ruza na Judica Losai.

Tazama video ifuatayo nikukumbushe habari hiyo:


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad