Hatimae Jeshi la Marekani Lakabidhiwa Aircraft Carrier Yake ya Kisasa Zaidi..Inauwezo wa Kukaa Miaka 50 Bila Kujazwa Mafuta..!!


Jeshi la majini la Marekani limekabidhiwa rasmi aircraft carrier yake ya kisasa zaidi USS Gerald R. Ford.

Jeshi hilo limesema kwamba carrier hiyo itafanyiwa majaribio mbalimbali baharini mpaka hapo 2020 ambapo itaanza kazi rasmi ndani ya jeshi hilo. 

Jeshi hilo pia limesema kwamba meli hiyo ya Gerald Ford ni ya kisasa zaidi ikiwa na mifumo mingi mipya yenye teknolojia ya juu, kubeba ndege nyingi zaidi,pia mfumo mpya wa kurusha ndege utasaidia kuongeza ufanisi wa jeshi hilo katika operesheni zake kwa zaidi ya mara tatu. 

Meli hiyo iliyokabidhiwa May 31 ilitarajiwa kua tayari September 2015,huku ikigharimu dola bilioni 12.9 badala ya dola bilioni 10.5 ikiyokadiriwa hapo awali. 

Nini kipya kwenye USS Gerald R. Ford?! 

1.Mfumo mpya wa kidijitali ambao unawezesha meli kuhudumu wafanyakaz wachache kulinganisha na carrier nyingine mfano; Nimitz 

2.Mfumo mpya na wa kisasa wa radar (Dual band radar) kuiwezesha kudetect vitisho kwa haraka na pia kwa umbali mrefu. (Mfumo huu pia unapatikana kwenye USS Zumwalt) 

3.Mfumo mpya wa kurushia ndege Electromagnetic Aircraft Launch System ambao huwezesha ndege nyingi kutumia mda mchache zaidi kuruka na kutua ukilinganisha na mifumo ya sasa

4.Uwezo wa kubeba hadi ndege 90 ikiwemo F-35C Lightning II. 

5.Radar cross section ndogo hivyo kuifanya kutokuonekana kirahisi kwenye radar za adui

6.Mifumo mipya ya kujilinda (SAMs), nk

7.Reactor mpya ya nuclear (A1B reactor) ambayo inaarifiwa kua na nguvu mara tatu zaidi ya ile inayotumika kwenye Nimitz (A4W) ambayo huzalisha megawat 190(190MW). Hivyo hii mpya ya Ford itakua na uwezo wa kuzalisha megawatts 570 (570MW).

Aircraft carrier hii inatarajiwa kutumika kwa kipindi cha miaka hamsini bila kujazwa mafuta huku ikiwa na mfumo wa Open Architecture kwa ajili ya uboreshaji zaidi huko mbeleni.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad