IGP Sirro Ataja Vipaumbele Vyake..Adai Haki Lazima Itatoa Majibu..!!!


Jeshi la Polisi linakabiliwa na changamoto mbalimbali.

 Kukosa ushirikiano kutoka kwa wananchi, malalamiko ya wapinzani, ujambazi, mauaji mkoani Pwani, rushwa, raia kujichukulia sheria mkononi na tabia za waendesha pikipiki za abiria ni baadhi ya changamoto nyingi zinazofahamika.

Lakini, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro amechagua masuala matano tu ya kuanza nayo.

Rushwa, bodaboda kutotii sheria na kujihusisha katika uhalifu, uchelewaji upelelezi wa kesi, wananchi kuchukua sheria mkononi na mauaji katika wilaya za Mkuranga, Rufiji na Kibiti ni mambo ambayo IGP Sirro ameahidi kuanza nayo.

“Kuna kikundi cha watu wachache ambao wanafikiri wanaweza kufanya ule mkoa usiwe na amani,” alisema Sirro jana katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu aapishwe kuwa mkuu wa chombo hicho cha dola mwanzoni mwa wiki.

“Lakini niwaambie kwamba siku zote haki lazima itatoa majibu na niwahakikishie Watanzania kwamba suala la Ikwiriri na Rufiji ni la muda tu.”


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad