Je Unajua Marehemu Ivan Don Alipotajirikia...Hii Hapa Historia Yake Fupi Itakayo Inspire Wengi

Ivan Don
RIP Ivan Don

Moja kati ya watu waliopata kuniinspire ni huyu Ivan - huyu jamaa nilimfahamu tangu hata Zari hajaachana nae... Jamaa alizamia kuingia SA kwa shida sana, alitoka UG akiwa masikini wa kutupa, hata alivyofika mpakani Zambia ama Zimbabwe (sikumbuki vzr) alikamatwa kwa kukosa vibali, lkn mwisho wa siku akatusua.

Baada ya kuingia SA akapambana sana sana sana ktk kile ambacho alikijua zaidi, huyu jamaa alikua daktari wa jadi "Mganga" - but very focused. Aliweza kuwatibu watu wazito sana akiwemo Mke wa Thabo Mbeki, alipooanza kupiga pesa za kibabe akawa anawaleta wauganda kutoka kijijini kwao anawatrain anachokijua kisha anawaachia clients wake.

Baadae akaanza kumiliki vitu vyenye akili, akaanzisha Brooklyn College ambayo inahusu sana mambo ya nursing, madini, uongozi na utawala, pamoja na technology. Jamaa baadae akarudi kuwekeza Uganda akajenga 4 star hotel njia ya kuelekea kijijini kwao, akajenga nyumba 2 huko kijijini kwao Manyonyo. Kisha akarudi SA akajenga Pretoria na Sandton (haya ni maeneo ya ushuani hasa).

Baada ya yote hayo akaona yupo vzr akaamua kuanzisha philanthropy (kutoa misaada) - hapa ndio mwanzo wa Rich Gang, akajenga orphanages 2, 1 SA na ingine UG... akawalea watoto yatima na wale waishio mazingira magumu. Akawa anatoa misaada sana kwa wamama ambao ni single parents nk, hata kabla hajafa alitoka UG akatoa misaada sana...

Na pia yeye alijulikana kama mwenyekiti wa waUG nchini SA, mUG yeyote akifika SA afu akawa hana dira basi akifika kwa Ivan anapata msaada, anapewa michongo na guidance ya kupiga pesa.

Jamaa kafariki na moyo wake... kafariki watu wanampenda... hana ugomvi na mtu, sijawahi kusikia akiwa na kashfa yoyote ya kulaghai, kutapeli, kunyanyasa nk. Yani alikua ni mtu safi sana... kafariki mapema sana... alikua humble sana, kwa familia yake alijitoa sana awe baba bora... Wanawake tunawajua akili zao - siwezi zungumza sana lakini Zari dada'ngu sijui kilitokea nini akashindwa kuelewana na Marehemu na Kumuacha.

Rest in peace rich gang president.

By ONTARIO

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad