James Mbatia: Rais Magufuli Ndiye Alipitisha Mikataba Bungeni kwa Ndio za Mia kwa Mia..!!!!


Nlikuwa namsikiliza Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi akutoa maoni juu ya Report zilizotoka za Mchanga wa Madini. 

Amesema Watanzania tuwe Watulivu na tujue Tanzania sio Kisiwa. Amepongeza nia nzuri ya Rais Magufuli. 

Amesema kinachotakiwa sasa kabla ya Mambo yote, wabunge Wapewe Elimu ya Madini na Elimu ya Soko la madini ili tusirudie Makosa tuliyoyafanya. 

Amesema kipindi Mikataba ya madini na Sheria zake zinapitishwa, rais Magufuli alikuwa bungeni na alipitisha sheria hizo asilimia mia kwa mia huku akishangilia. Hali hiyo imefanya wabunge kupitisha mambo mengi yasiyo faa hasa madini tangu 1998 hadi elfu 2010 na madiliko yote yalikuwa yanafanywa kwa jaziba. 

Rais Magufuli alikuwa bungeni miaka 20 ambayo ndo sheria hizo zimepitishwa. Walikuwa wanajibu ndio tena kwa kushangilia. Hivyo haipendezi kama taifa turudi huko tena. 

Wanasheria wetu wafanye kazi usiku na mchana kuangalia Sheria za Kimataifa zipoje na Sheria zetu zipoje

Rais ana nia njema, tujipe muda, tuwe watulivu.. Tusifanye tena kwa mihemko kama huko nyuma. Japo wanasema walifanya kwa nia njema. 

Nasikia wabunge wanasema repoti hizi ni za upande mmoja, tujipe muda wa kusikiliza upande wa pili. 

Tutumie nguzo tatu katika Wimbo wetu wa Taifa; Nguzo ya Hekima, Nguzo ya Umoja wa kitaifa na nguzo ya Amani ya Taifa letu kijiweka katika ramani ya dunia. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad