Wananchi Bukombe Waomba Rais Magufuli Aongezewe Muda wa Kukaa Madarakani

Wananchi wa vijiji vya Bulangwa na Katente mkoani Geita,wameliomba Bunge la Tanzania kufanya marekebisho ya muda wa ukomo wa urais kutoka miaka kumi ya sasa hadi miaka ishirini ili kumuwezesha Rais Dk.John Pombe Magufuli kuendelea kubakia madarakani.

Wananchi hao walitoa ushauri huo jana katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na mbunge wa jimbo la bukombe mh. Dotto biteko kwa ajili ya kumpongeza Rais Dk.John Pombe Magufuli kwa namna alivyosimamia sekta ya madini,mkutano ambao ulihudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Geita mjini Mh.Costantine Kanyasu.

Akiwahutubia wananchi,Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Nishati na Madini Mh. Dotto Biteko,alisema kazi ya kupigania rasilimali za taifa inayofanywa na Rais Dk. John Pombe Magufuli si ya lelemama,huku Mbunge wa Jimbo la Geita mjini Mh. Kanyasu akisema serikali ya awamu ya tano haiwachukii wawekezaji, bali inawachukia waporaji wa raslimali za nchi.

Ripoti ya kamati ya pili ya mchanga wa madini wa Makinikia,iliyowasilishwa Juni 12 mwaka huu kwa Rais Magufuli na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Prof.Nehemiah Ossoro ilibaini taifa kupoteza shilingi Trilioni 252 kupitia usafirishaji wa mchanga wa madini ya makinikia nje ya nchi kuanzia mwaka 1998 hadi kufikia mwaka huu,huku ikiwahusisha baadhi ya mawaziri wa zamani wa nishati na madini waliohusika kuingia mikataba mibovu iliyoisababishia serikali hasara.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mpaka nione kama anakwrndaje. Bila woga, atende haki, uhuru wa waandishi, bila kujali cheo, adhabu kali kwa wahusika. Msitupake mafuta kabla hatujsona anawahusisha watanzsnia wote. Anapokea ushauri, asiwr pupa kukubali machache, ajue wazungu wezi. Na wanaakili, awahudishe wenue skili wanaoweza kabiliana na mafisafi na mabepari kufuata sheria nauzoefu. Sijanunulika bado. Nyinyi hamjuo ugumu wa manbo hays. Msigieni, ndiyo, bado nangoja kiona mengi. Bola wapinzani, hatungefika hapa. Naona wabunge wa CCM ni sifa tupu kwake . Sifa zisizo na maelezo. Wabunge wa CCM wasipotoshe umma. Wawe serious kwa haya. Wengi hawafai na hawana maarifa ni mizigo tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hata kuandika vizuri umeshidwa. Magu ata akiongezewa muda wa uongozi ni sawa kabisa. Kwani ni Raisi anaejituma na kufanya kazi yake, si mwenye tamaa ya kulibia Taifa lake. Kama wanavyofanya viongozi wengi wa bara hili, Bali ni mtu mwenye kupenda maendeleo na uchungu wa nchi yake kwanini? Ni masikini mpaka Leo, wakati kunna kila Aina ya utajili ndani yake. kunna nch kama South Korea wamepiga hatua ya kiuchumi na ni matajiri sanaa tu na wenye maendeleo, tena kwa muda mfupi tu, na wala hawana uchumi asilia kama sisi, tunaombiwa IQ ndogo, uchumi asilia umejaaa kibao kila kona lakini tu wamasikini wa kutupwa na tunawaza eti kusaidiwa na nchi matajili, wakati wanatuona wajinga, hatuna interligent Qurty, hatupendi kufanya kazi tumekalia ombaomba, saidia baba wakati Mali tunazo tumezikalia, Lakini yote hii ni kutokana na uongozi mibofu ya bara hili la Afrika. Viongozi wasiojua wajibu wao, hawana vision wanaopenda corruption wao wapo wapo tu.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad