Rais Magufuli ameyasema hayo leo (Jumatano) Ikulu baada ya kukutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Barrick ya nchini Canada, Profesa John Thornton.
Barrick Gold Corporation ni kampuni mama ya kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia.
“Nimesoma ripoti zote mbili hakuna mahali ambapo Mzee Mkapa na Mzee Kikwete wametajwa, vyombo vya habari viache kuwachafua hawa wazee, wamefanya kazi kubwa ya kulitumikia Taifa letu, viwaache wapumzike,” amesema Rais.
Ameonya viongozi hao kuhusishwa katika taarifa za kamati mbili za uchunguzi wa madini yaliyo katika makontena yenye mchanga wa madini (makinikia).
Tawire mkuu, umesomeka......
ReplyDeleteTunaomba tuungane Tanzania nzima. Naomba tuungane kabisa. Yeyote bila kujali cheo chake kwa kuiingiza nchi na watu wake kwenye mikataba hii mibovu wakijua akina mama wanakufa hospitali wanapojifungua kwa kukosa huduma . Na pesa hizi za wananchi waliowapoteza wake, watoto, mama zao hili ni kosa la jinai. Watu fungeni mikanda na mlijadili hili kwa undani. Watu wanapoteza maisha ambayo huwezi kurudisha wala kulipa. Kwa wahusika wote wa ngazi toka raisi mpaka diwani naomba sana wasiwe na kinga yoyote. Tanzania ijue, na Wananchi wajue, ni sisi wenyewe kwa kukumbatiani ni nyasi wadogo, watu wa vijijini hasa karibu na maeneo hayo. wengine hawana maji safi ya kunywa, wanaka chini watoto kusoma ambao ni taifa la kesho mtoto anakosa elimu kisa makosa makusudi ya Raisi je kinga ya nini Raisi Wangu. Je hizi familia maelfu ya Watanzania utawajibu nini? huwaonei huruma. Huruma ni kuwaadhibu wote waliohusika. inabidi moyo na na nguvu za mungu kutenda haki.Wote tukimuomba Mungu wa kweli atatuambia tumieni madaraka yenu vizuri kwa ajili ya maskini na wasiojua na wasio na elimu. Ni hivi ndivyo utamcha Mungu wa kweli na atakubariki zaidi, kukulinda, kukupa ushujaa wa kweli. ili uifanye kazi yake vizuri bila woga. Mungu ibariki Tanzania na vingozi wote watendao haki. Mungu ibariki Afrika isirudi kule nyuma tulikouzwa na shanga leo tunaibiwa dhahabu kwa hongo na ufahari wa wachache. Tanzania haijajengwa hivi. Turudi kule Baba wa Taifa Nyerere alivyosema, acha dhahabu ardhini mpaka elimu zetu zitakapoweza.Haiozi.
ReplyDelete