Winga wa kimataifa wa Uholanzi aliyekuwa anaichezea KRC Genk kwa mkopo akitokea FC Basel ya Uswiss Jean Boetius leo June 23 2017 ametangaza rasmi kuondoka na kurudi katika club yake ya Feyenoord ya kwao Uholanzi na atapata fursa ya kucheza Champions League msimu ujao.
Boetius akifurahia na Samatta baada ya kufunga goli
Jean Boetius anarudi kuichezea Feyenoord ya kwao Uholanzi ambao ndio Mabingwa wa Uholanzi baada ya kucheza KRC Genk ya Ubelgiji ambayo pia inachezewa na mtanzania Mbwana Samatta, Feyenoord ndio timu iliyomlea Boetius toka akiwa na umri wa miaka sita na mwaka 2015 ndio akaondoka kwenda FC Basel na kudumu kwa misimu miwili.
Winga huyo ambaye yupo katika kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi amerudi katika club hiyo baada ya kucheza KRC Genk kwa muda wa miezi sita toka ajiunge nayo mwezi January 2017, kutumia ukurasa wake wa instagram Boetius ameandika “Home is where the hearts is!” akiwa na maana “Nyumbani ni sehemu ambayo moyo wako ulipo!”