KIMENUKA..Shirika la Wanawake Barani Afrika Limemtaka Rais Magufuli Kuomba Msamaha


Matamshi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kutoendelea na masomo yamezua gumzo kubwa na mijadala mbalimbali ndani na nje ya nchi.


Shirika la wanawake barani Afrika limemtaka Rais Magufuli kuomba msamaha kutokana na matamshi yake aliyoyatoa akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Pwani kuwa mwanafunzi atakayepata ujauzito katika utawala wake hataweza kuendelea na masomo.


Hata hivyo, katika sheria iliyopitishwa mwaka 2002 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu suala la mtoto wa kike kupata ujauzito akiwa shule inaruhusu kufukuzwa shule na kifungo cha miaka 30 kwa yule aliyesababisha ujauzito huo.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wabongo mtambue kuwa huyu Rais hakurupuki hovyo hovyo bila ya kupitia KATIBA na ilani ya chama tawala ona sasa katiba inasemaje?Hata hivyo, katika sheria iliyopitishwa mwaka 2002 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu suala la mtoto wa kike kupata ujauzito akiwa shule inaruhusu kufukuzwa shule na kifungo cha miaka 30 kwa yule aliyesababisha ujauzito huo.

    ReplyDelete
  2. Tatizo wnawake kila kite wao wanaona wanaonewa, ndio kunna matatizo menig ambayo mwanamke anaweza kukumbana nayo asa katika umri Huo wa kwenda shule, ikawa kwa kujitakia au kwa matatizo tu, ambayo yamesababishwa na wanume wenye Tabia mbaya, au tamaa, ILa hili jambo likirusiwa itakuwa tabu Hasa kwa nchi zetu ambazo bado ni masikini wa kiuchumi, kwani itakuwa kama kuruhusu mashuleni kubeba mimba wakitarajia mbona wataendelea na shule kama kawaida, wala hawataogopa hata kufanya ufuska na unzinzi iwe mashuleni au nje ya mashuleni, itakuwa kama kuruhusu ufuska na uzinzi kwa hao wasichana wanafunzi,

    ReplyDelete
  3. Namkubali sana mueshimiwa maghuful licha yakwamba nina mashaka makubwa na watu anaowaongoza..No doubt hapana shaka hata kidogo yakwamba watanzania wengi hasa wanaojifanya wamesoma au wanaoishi mijini ni watu wa hovyo kupita kiasi. Sisi tunaoishi nje huku tuna kazi kubwa ya kujibu masuali kutoka kwa watu wa mataifa mbali mbali wakiuliza kama kweli Magufuli ni mtanzania? Au mwafrica halisi au labda miaka mingapi aliishi nje kabla yakuamua kurudi nyumbani na kuanza kufanya kazi kwa vitendo na uadilifu kama viongozi wa nchi zilizoendelea. Hao wanawake wa Africa na viongozi wake ni watu wa hovyo na tope kabisa . Na tatizo ni lile lile Africa hakuna viongozi sasa anapotokea kiongozi wa kuwango cha Magufuli maamuzi yake lazima yawachanganye wenye akili ndogo. Kuhusu suala la Magufuli kuwa mkali katika wanaopata ujauzito kutorejea shule, jibu ni dogo tu muheshimiwa Magufuli anapambana na kuzuia mimba za utotoni kwa watoto wa kike kitu ambacho ndicho kinachowapelekea wanawake wengi hasa katika nchi za Africa kuwa na maisha duni baadae. Sasa hapo utaona uduni wa akili wa hao wanaotaka kuombwa radhi. Walitakiwa kumpongeza sana kwa kauli yake ile badala ya blah blah za hovyo.

    ReplyDelete
  4. Yaani wanashabikia kwa mwanafunzi kubeba mimba shule loooohhh!,,, Wonder Shell never end in Africa or Tanzania mmmmmh stupid people wanaojionawamelimika kumbe ni dumbas people

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad