KIMENUKA:Video ya Polisi Wakiwapiga Walemavu DAR Yawakera Wengi...Itazame Hapa


Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam jana lililazimika kutumia mabomu ya machozi kukabiliana na kundi la walemavu wa viungo waliokuwa wamefunga barabara ya Sokoine wakishinikiza kuonana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala.

Mabomu hayo hayakusababisha wakati mgumu kwa walemavu hao waliokuwa wamefunga njia tu bali hata kwa watumiaji wengine wa barabara hiyo.

Walemavu hao walitaka kuonana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kumueleza kero wanayokumbana nayo ya kukamatwa na Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni alisema kuwa walilazimika kutumia mabomu hayo kama njia ya kuwatawanya na kuwa hadi sasa wanawashikilia watu 40  kwa kosa la kufanya mkusanyiko kinyume na sheria.

Alisema kuwa walilazimika kutumia njia hiyo ya mabomu baada ya watu hao kupewa amri mara tatu ya kutawanyika na kukaidi. Hivyo akasema utumiaji wa mabomu hayo ulifanyika ili kurahisisha ukamataji wa wananchi hao waliokaidi amri ya Polisi.

Aidha, licha ya kiongozi huyo kusema hivyo, watu mbalimbali kikiwemo na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimelaani nguvu iliyotumiwa na polisi katika zoezi hilo na kusema ni nguvu kubwa ambayo haikuhitajika kukabiliana na walemavu ambao hawawezi kupambana na Polisi.

Wengi waliotoa maoni yao kuhusu video hii kwenye  mitandao ya kijamii wamemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba kuwachukulia hatua Polisi hao wanaoonekana wakiwapiga walemavu hao na kuwaingiza kwenye magari ya Polisi kwa kutumia nguvu kubwa.

ITAZAME HAPA CHINI:


Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwàni lengo lao kuu ilikia wahitaji kitu gani?. Kutoka kwa huyo mkurugenzi.
    Swali najiuliza bila kupata majibu. Walishawahi kuoeleka maombi yakua wanataka mazungumzo na yeye nakama walipeleka walishajibiwa nakama walijibiwa walishambiwa lini au welikwenda kwa utashi wa vijiweni
    Kama hawajafata hizo taratibu kilicho wakuta nimuafaka kwasababu tiisheria bila ya kushurutishwa kwani sheria aina maumbile wa jinsia

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad