KKKT Waliamsha DUDE...Wamtaka Rais Magufuli Akamilishe Katiba Mpya

ASKOFU mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Blaston Gaville, amemuomba Rais Dk. John Magufuli kumalizia mchakato wa kuandikwa kwa Katiba mpya ulioachwa na mtangulizi wake.

Akizungumza baada ya kuwekwa wakfu Askofu Gaville na msaidizi wake, Himidi Sagga, katika ibada iliyofanyika juzi katika Viwanja vya Shule ya Msingi, Gangilonga, alisema Wakristo na Watanzania kwa ujumla wana imani kubwa na Serikali ya Dk. Magufuli na ni matarajio yao kwamba mchakato wa kuandika Katiba mpya utamalizwa kama lengo lilivyokuwa.


Askofu huyo alisema Dayosisi ya Iringa inatoa mwaliko kwa vyama vyote vya siasa na jamii nzima ya Watanzania kuendeleza kukuza tunu ya ushirikiano na moyo wa kizalendo ili kuwa na maendeleo yenye tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Katika ibada hiyo, Askofu Gaville alieleza kuwa wanatiwa moyo na jitihada zinazoendelea kufanywa na Dk. Magufuli katika kufufua uchumi na kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika kwa manufaa ya Watanzania wote na

kwa kufanya hivyo, ni faraja kubwa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

“Kweli nasema nchi yetu ina wanyonge wengi kuliko wenye nguvu, tunatiwa moyo na rais na Serikali yake tunapoona wanatetea wanyonge,” alisema Askofu Gaville.

Hata hivyo, askofu huyo aliiomba Serikali iangalie upya suala la kodi kwa mashirika ya dini kwakuwa baadhi ya kodi wanazolipa ni kwa kuendeleza elimu kupitia vyuo vya ufundi.

“Katika kuunga mkono jitihada za Serikali, kanisa linasaidia watoto masikini wapate haki yao ya elimu, tunaomba Serikali isituingize katika kundi la watoto wanaotoka katika familia zenye uwezo kwa sababu wanasoma shule binafsi.

Chanzo: Mtanzania

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad