Kuna hili suala limekuwa likitumiwa sana na Simba kwenye kulaghai wachezaji masikini wa Kitanzania.
Wenyewe wanasema "Ukicheza Simba ni sawa na kuwa njia panda ya ULAYA".
Nimemsikia yule beki wa kushoto aliyetoka Mbao FC someone Mlipili akihojiwa. Anasema kuwa amejiunga simba kwa kuwa unajua ni njia panda ya kwenda ULAYA.
Nikacheka na kujiuliza ' Hivi huyu dogo nani amemuaminisha kuwa ukicheza simba ndio una uhakika wa kuja kucheza Ulaya?. Hivi ni kweli ameahindwa kujiuliza yaliyomkuta Mgosi ambaye alijikuta akitupwa kwenye misitu ya DR Congo? Haoni jinsi Mkude anavyoendelea kuzeekea pale, amuoni Zimbwe JR na ubora wake wote hajawahi hata kuitwa Somalia akafanye trial?. Ni nani amemuaminisha kuwa akicheza pale simba kuwa yeye anaweza kufanikiwa kucheza soka la nje. Si watu wengine bali ni viongozi wa simba wanao walaghai hawa wachezaji.
Huwaga najiuliza ni wachezaji wangap ( kushinda Yanga SC) ambao Simba imewalea na kuwakuza mpaka wamefikia ubora wa kupata nafasi nje ya nchi?
Okey! wengi wanasema Samatta amepata nafasi ya kwenda nje kwa sababu ya kucheza simba, ila ukweli halisi ni kwamba kwa kipaji alichonacho Jamaa ni dhahiri asingekaa Bongo hata kama asingechezea simba. Licha ya kuwa pale simba alipita tu kwa nusu msimu.
Kuna jamaa nimemuuliza maswali kadhaa, kwanza "ni mchezaji gani ambayo simba wanajivunia kapitia simba na kupata nafasi nje ya Nchi?"
Akajibu "Samatta."
Nikamuuliza "|akini mbona YANGA amepita mtu kama NONDA"?
Hakuweza kuendelea kujibu kwa hoja, lakini ki uhalisia unajiuliza kwanini simba wanajisifu kutoa wachezaji nje ya nchi ikiwa hawajatoa wachezaji kuizidi Yanga.?
Wapenzi wengi wa simba hawawezi kujibu hili swali kwa ufasaha.
Hii inadhihirisha ni njama za ulaghai za baadha ya viongozi wa simba kuwafanya wachezaji waache kufuata ndoto zao za kutwaa MATAJI na kubaki simba wakiamini ipo siku watacheza ULAYA.