Lissu: Kama ACACIA ni Wezi, kwanini Polisi Wamewapiga Mabomu Wananchi wa Tarime?

Lissu: Kama ACACIA ni Wezi, kwanini Polisi Wamewapiga Mabomu Wananchi wa Tarime?
"Tumeambiwa Acacia ni wezi, hawana leseni ya uchimbaji, hawajasajiliwa nchini. Wananchi wa Tarime walipoamua kuchukua hatua wamepigwa mabomu.

Kama Acacia ni wezi na hawajawahi kuwa na leseni kwa nini polisi wa Magufuli wanawapiga wananchi wa Tarime mabomu? Nani anayetetea wezi hapa

Nani mchochezi kati ya Rais aliyelia hadharani kuwa Acacia wezi, na mbunge wa Tarime aliyewaambia wananchi kuchukua hatua dhidi ya wezi hao?"

Tundu Lissu amehoji hayo baada ya Polisi kuanza kumtafuta John Heche kwa kuchochea wananchi wavamie Migodi ya dhahabu.

Akiwa bungwni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche alifunguka na kusema kwa kuwa Rais Magufuli kupitia ripoti ya pili ya mchanga amesema kampuni ya ACACIA ni feki na haipo basi yeye anawaambia wananchi wa jimbo lake wajiandae kuingia mgodini kuchukua kila kitu.

Heche alisema hayo bungeni na kudai kuwa atasimamia zoezi hilo na kuhakikisha kuwa ndege za kampuni hiyo zikitua mgodini kwa ajili ya kubeba madini basi zinapigwa mawe kwa kuwa wananchi wa jimbo lake la Tarime ambapo hiyo migodi ipo wameumizwa sana kusikia hiyo kampuni inayochukua mali zao ni feki na hewa.

"Kampuni ile ya ACACIA Rais amesema feki na hakuna 'formula' ya kukamata mwizi mlisema wenyewe, formula ya kukamata mwizi ni kupambana naye sisi hatutaruhusu madini yatoke pale ndege ikitua itapigwa mawe, magari yao tutayakamata kwanza tunawadai fidia nyingi kweli kweli pale Tarime. Mhe. Spika sisi tulitegemea Mhe. Rais aseme madini yasiondoke nchini mpaka mambo hayo yote yapitiwe, tutazuia mchanga madini yanaondoka. Rais amesema ACACIA ni mwizi wewe unataka utaratibu wa kukamata mwizi Tarime, sisi watu wetu wameumia sana na maji ya sumu, ng'ombe wamekufa, watu wamepigwa risasi kwa mujibu wa ripoti ya Waziri wa Nishati na Madini watu wa Tarime zaidi ya 64 wameuawa pale mgodini" alisema Heche

Mbali na hilo John Heche alisema kuwa kama serikali itamkamata kwa maamuzi ambayo atafanya basi Watanzania watajua kuwa serikali haipo tayari kupigana vita hii ya kupigania rasilimali za nchi hii, hivyo amewataka watu wa jimbo la Tarime wajiandae na kuanza maandalizi ya kupigania rasiliamali zao ili waone kama serikali itapeleka jeshi la polisi kulinda mali za wezi hao.

Kwa siku tatu mfululizo wananchi wa Tarime wamekuwa wakivamia Mgodi wa dhahabu usiku na mchana huku Polisi ikiwapiga Mabomu na kuwatawanya.

By Figganigga/Jamii Forums

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. unaweza ukawa msomi but usiwe na akili ya kuelewa moja jumulisha moja ni ngapi? tundulisu wewe ukiwa kama raisi wa wanasheria lakini huna uelewa maana sasa tofautisha kati ya acacia mining plc. na north mara gold mine ltd ndo utajua kwanini heche anatafutwa kwa uchochezi. mbona mnapenda kukuza mambo sana nyie>

    ReplyDelete
  2. Nyinyi eote mliotoa maoni hakuna kitu. Anachokisema lisu ni hiki. Hawa watu no wezi. Hawana hata leseni. Inamaana wanachukua madini bure kabisa. Sielewi kwa bipo waendelee kuchukua fhahabu tena. Wanaiba mnaelewa hii.na ni kama hawsna leseni hawa watu hawana haki youote kile mgodini. Ule mgodi so wao.kwanza hawana hski kuja tena Tanzania. Ingekuwa nvhi nyingine wasingrpewa hata bisa tena kuingia mpaka wailipe nchi kwanzs. Inatia aibu kwa nchi kitokujua sheria zao. Ni sibu kubwa sans. Hibi mnawaogopa wazungu wezi? Ingekuwa Mtanzania umrfanya hilo kwso umeshawekwa ndani kwanza. Bipi hizi sheria na kutokukazia mnayotarajia. Maneno matupu hayavunji mfupa. Nysnganya sehemu isitumike tena.nyi watanzania wsnyonge msiojua sheria mnazifi kusifia msmbo hsta hamuelewi mnachosifis. Hakijaisha na hamna uhakika kama mtslipwa. Ni maneno tu mnatulia. Hamna uchungu na mali zenu. Mnasibisha pia.vichwa vimejaa maji matupu. Hsmtsjikomboa kama hamna elimu au elimu za ubabaishaji tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad