Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amefunguka na kuweka wazi kuwa Chama Cha Wananchi ( CUF) hakina mgogoro wowote na Profesa, Ibrahim Lipumba na kudai kuwa kiongozi huyo si mwanachama wa CUF bali ni mwanachana wa Jaji Mutungi.
Maalim Seif Sharif Hamad amedai Lipumba si Mwenyekiti Chama cha Wananchi (CUF) na kudai kuwa mkutano Mkuu wa CUF ulishamuondoa siku nyingi lakini yeye mwenyewe alishajiuzulu nafasi hiyo.
"Wengi wanaulizia mgogoro huu na Lipumba sisi CUF hatuna mgogoro na Lipumba, Lipumba si mwanachama wetu kabisa kabisa, Lipumba ni mwanachama wa jaji Mutungi na Mwenyekiti wa jaji Mutungi lakini siyo mwanachama wala Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Mkutano mkuu umeshamuondoa Mwenyekiti si Mwenyekiti kwani alishajiuzulu mwenyewe na Baraza Kuu lilimfukuza uanachama" alisisitiza Maalim Seif
Mbali na hilo Maalim Seif aliwapa mbinu wabunge na viongozi wa kisiasa hususani wapinzani, jinsi ambavyo wanaweza kukutana na watu wapiga kura wao na kuweza kufanya siasa katika mazingira hayo hayo watakayokutana nao.
Maalim Seif amedai kuwa Lipumba ni mwanachama na Mwenyekiti wa jaji Mutungi kwa kuwa ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa nchini inamtambua Profesa, Ibrahim Lipumba kama Mwenyekiti CUF na mwanachama wa CUF.