Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya watu waliojaribu kushiriki gwaride hilo na kuwakamata baadhi yao.
Mamlaka inasema imechukua hatua hiyo ili kuzima tishio la makundi yanayopinga serikali kutumia gwaride hilo kuzusha vurugu.
Wanaharakati wa kutetea haki ya wapenzi hao wa jinsia moja wamepuuzilia mbali madai hayo na kuongezea kuwa serikali inatumia vigezo hivyo kama sababu ya kuminya uhuru wa watu hao.
Wanamshutumu Rais Recep Tayyip Erdogan anayegemea maadili ya kiislamu kwa kujaribu kuliendesha taifa kwa kutumia mtazamo wake binafsi juu ya masuala fulani katika jamii.