Ni wazi kabisa kuwa Ugaidi ni Uadui mkubwa sana katika dunia hii, Pia ni Upumbavu na Dhambi.
Nimefurahi sana kusikia hatua iliyoamua kuchukuliwa na Serikali kuwa watapeleka "Wanajeshi" katika Wilaya za Mkuranga na Kibiti ili kuwadhibiti hao Magaidi walioua viongozi wa vijiji, mapolisi na wananchi.
Mwaka 1998, serikali ilichukua hatua kama hiyo ya kuwapeleka wanajeshi wilayani Ngorongoro wakisaidiana na Wamasai ili kupambana na majangili ya kisomali (baada ya mapolisi kushindwa kuwathibiti na OCD wao kuuawa na majangili hayo)
Mpaka leo hii Ngorongoro kumetulia tuli.
Magaidi waliotajwa rasmi wapo 11 na waliotiwa mikononi ni wanne.
Imethibitika kuwa Magaidi hao wote ni waumini wa dini ya kiislam hivyo wengi kuhusisha ugaidi wao na imani ya dini yao.
Zaidi baadhi ya wananchi wa wilaya hizo walihojiwa na kusema kuwa watu hao wamekuwa wakisema kuwa wanawachukua vijana wao na kuwapeleka Somalia kwa ajili ya mafunzo mbalimbali ya kujikwamua kiuchumi.
Hata hivyo, haijathibitishwa kwa asilimia zote kuwa walipata support za kiimani ya dini yao.
Wafuatao ndio wahusika wa ugaidi waliotajwa:-
1) Faraj Ismail Nangalava
2) Anaf Rashid Kapera
3) Said Ngunde
4) Omari Abdallah Matimbwa
5) Shaban Kinyangulia
6) Haji Ulatule
7) Ally Ulatule
8) Hassan Uponda
9) Rashid Salim Mtulula
10) Sheikh Hassan Nasri Mzuzuri
11) Hassan Njame
Source: Gazeti la Jamhuri trh 13-19.